A new AI capability that delivers analysis-ready Media Intelligence. More than just a product launch, this is a shift in how communications teams monitor, understand and act on media coverage.
IPP Media is a private company, held under IPP Group and based in Dar es Salaam, Tanzania. IPP Media comprises nine newspapers, which are published in both English and Swahili, three television stations, and four radio stations (Radio One, SkyFM, Capital radio and East A.... Source
Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imesema ujenzi wa moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST utachangia kuongeza uwajibikaji, uwazi na ufanisi kwenye mnyororo wa ugavi.
By Mwandishi Wetu , Nipashe Published at 01:01 PM Apr 08 2026 Picha Mtandao Bei za mafuta soko la dunia zashuka BEI ya mafuta katika soko la dunia imeshuka baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukubali kusitisha mapigano kwa wiki mbili na Iran, na kuzua matumaini kwamba meli zaidi za mafuta zitaweza kupita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz hivi karibuni.
By Paul Mabeja , Nipashe Published at 05:06 PM Apr 08 2026 Picha Mtandao Rais Samia apunguza idadi magari katika misafara yake RAIS Samia Suluhu Hassan, ametangaza kupunguza idadi ya magari kwenye misafara yake mbalimbali ya kikazi ikiwa ni moja ya mkakati wa kupunguza matumizi makubwa ya mafuta serikalini. Samia, amesema hayo leo Ikulu ya Chamwino, baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali wa serikali aliowateuwa kushika nafasi mbalimbali hivi karibuni.
By Paul Mabeja , Nipashe Published at 02:51 PM Apr 08 2026 Picha Mtandao Waitaka serikali kupunguza matumizi ili kuongeza ruzuku ya mafuta MBUNGE wa Ikungi Elibariki Kingu, ameishauri serikali kuondoa matumizi yote ambayo hayana umuhimu ikiwemo posho na vikao visivyokuwa na ulazima kunzia mwezi Aprili hadi Julai mwaka huu, ili fedha zitakazookolewa ziwekwe kwenye ruzuku ya mafuta.
KATIKA biashara ya kimataifa, kazi ya uwakala wa forodha imekuwa mhimili muhimu kwenye kuhakikisha mizigo inaingia na kutoka nchini kwa kuzingatia sheria na taratibu za kodi. Hata hivyo, kwa miaka mingi, sekta hii imekumbwa na changamoto lukuki, kuanzia migogoro ya malipo kati ya mawakala na wateja, ushindani usio wa haki, hadi ukwepaji kodi uliokuwa unalinyima taifa mapato.
Wanasayansi wanaanga ni miongoni mwa kundi linalofuatiliwa na kupewa udadisi mkubwa na wafuatiliaji wa taarifa za habari kimataifa. Wiki hii kwa mara ya kwanza ikipita zaidi ya miaka 50, binadamu ameweza kurudi mwezini kupitia Misheni ya Nasa ya Artemis II, iliyozinduliwa Aprili Mosi, mwaka huu. Inatajwa na wanasayansi kuwa safari yenye hatari zaidi, huku wanaanga wanne kati yao mmoja mwanamke, watafanya safari ya zaidi ya maili nusu milioni.
By Marco Maduhu , Nipashe Published at 05:22 PM Apr 02 2026 Picha: Marco Maduhu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya hesabu za serikali la baraza la wawakilishi Zanzibar (PAC) Kombo Mwinyi Shehe akizungumza katika ziara, mradi wa umeme jua uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar (PAC) imeiomba TANESCO kuongeza kiwango cha umeme kinachouzwa Zanzibar ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka.
By Thobias Mwanakatwe , Nipashe Jumapili Published at 12:52 PM Mar 22 2026 Picha: Mtandao Wadau wa ufugaji wa nyuki katika Mkoa wa Singida wameuomba Umoja wa Mataifa (UN), kuingilia kati na kusihi mataifa ya Marekani, Israel na Iran kusitisha matumizi ya silaha nzito. Wamesema kuwa kelele za milipuko na makombora katika vita zinachangia kuathiri kwa kiasi kikubwa ustawi wa nyuki na uzalishaji wa asali duniani.
By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili Published at 10:09 AM Mar 22 2026 Picha: Mtandao Rais wa Marekani, Donald Trump Rais wa Marekani, Donald Trump, ameipa Iran muda wa saa 48 kufungua tena mlango wa Bahari wa Hormuz, akisema isipofanya hivyo “ataiangamiza” kwa kuanza na mitambo yake ya umeme.
By Mwandishi Wetu , Nipashe Jumapili Published at 02:00 PM Mar 22 2026 Picha: Mpigapicha Wetu EU yatoa bilioni 1.3 kupambana na magonjwa yanayovuka mipaka Jumuiya ya Ulaya (EU), imetoa Euro 443,989 kwa taasisi nne nchini kwaajili ya mradi wa kutoa mafunzo kwa madaktari na wahudumu wa sekta ya afya kuhusu namna ya kudhibiti na kutibu magonjwa yanayovuka mipaka duniani.