YY Gushes Over GF's New Instagram Page The comedian has gone all out for Noela The comedian stunned Kenyans a few weeks ago by launching a new girlfriend days after revealing that he and baby mama Marya were no more Related Articles
Brandon Asiema
(He/Him)
As seen in:
Radio Jambo (Nairobi, Kenya),
Mpasho
Covers:
Sports, Current Affairs, Human Interest Stories, Politics
Journalist || Producer || Drone Pilot.
Articles by Brandon Asiema
Jukwaa la E-Citizen linaendeshwa kikamilifu na serikali kuu - Mbadi
Waziri wa hazina ya taifa na mipango ya kiuchumi John Mbadi amesema kuwa mfumo wa E-Citizen sasa unaendeshwa kikamilifu na serikali kuu kupitia mamlaka ya mawasiliano na habari ICT. Akizungumza mbele ya seneti asubuhi ya Jumatano tarehe 2 Oktoba, Mbadi alisema kuwa mamlaka ya ICT imechukua usimamizi wa E-Citizen katika mpangilio wa kimkataba utakaodumu kwa miaka 3.
Msajili wa vyama vya kisiasa aidhinisha chama cha INJECT Party chake Morara Kebaso
Harakati ya kusajili chama cha INJECT kama chama cja kisiasa nchini Kenya kinaendelea kupiga hatua. Jina la chama kilichobuniwa na mwanaharakati Kebaso Morara kwa jina chama cha kujumuishwa kwa haki ya kitaifa, mabadiliko ya kiuchumi na kiraia maarufu kama INJECT Party (Inclusion of National Justice, Economic and Civic Transformation) limekubalika.
Vipusa wa Kenya U17 watua nchi ya Jamhuri ya Dominican kwa kipute cha dunia
Timu ya wasichana chipukizi wa Kenya wasiozidi umri wa miaka 17 waliwasili katika nchi ya Jamhuri ya Dominican alfajiri ya Jumatano tarehe 2 Oktoba. Timu hiyo chini ya kocha Mildred Cheche inajiandaa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kombe la dunia FIFA ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17. Kipute cha kombe la dunia kitaandaliwa nchini Dominican kuanzia tarehe 16 Oktoba ambapo timu ya Kenya itashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza.
Empoli ya Serie A yammezea mate Timothy Ouma
Kiungo mkabaji wa timu ya taifa Harambee Stars Timothy Noor Babu Ouma maarufu kama Timothy Ouma sasa anavutiwa na timu kadhaa zanazoshiriki ligi kuu Italia, Serie A. Kinda huyo wa miaka 20, kwa sasa anatumikia timu ya Elfosborg inayoshiriki ligi ya Allsvenskan nchini Uswidi. Kwa mujibu wa mtaalam wa uhamisho wa soka Gianluca Di Marzio amesema kuwa Empoli ni mojawapo wa vilabu nchini Italia vinavyommezea mate mchezaji huyo.
Kenya ina wanagainakolojia 700 pekee
Mwenyekiti wa kamati ya afya katika bunge la kitaifa Dkt. Robert Pukose mnamo Alhamisi aliiambia bunge kuwa Kenya ina wanagainakolojia 700 kote nchini. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa barua iliyowasilishwa na wizara ya afya kwa kamati ya afya katika bunge la kitaifa tarehe 12 Agosti, 2024. Dkt. Pukose alisema hayo akiwasilisha majibu ya kamati anayosimamia kwa wabunge waliotaka kufahamu kuhusu hali ya ukosefu wa vifaa maalum vya kushughulikia wagonjwa wa Endometriosis.
Junior Starlets kupimana nguvu na Ureno matayarisho ya FIFA
Timu ya taifa ya wanadada wasiozidi umri wa miaka 17, Ijumaa watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Ureno kuanzia saa kumi na moja majira ya Afrika Mashariki. Timu hiyo chini ya uongozi wa kocha Mildred Cheche ipo nchini Uhispania kwa mazoezi ya ziada wanapojiandaa kushiriki mashindano ya FIFA ya wanadada wasiozidi umri wa miaka 17. Mechi hiyo itakuwa ya pili kwa Junior Starlets wakiwa nchini Uhispania baada ya kucheza mechi ya kwanza mnamo Jumatano dhidi ya Ciudad Deportiva Del Valencia.
Wizara ya michezo kuanzisha mashindano katika kambi za wakimbizi
Waziri wa maswala ya vijana, sanaa na michezo Kipchumba Murkomen amesema kuwa wizara ya michezo itaanzisha michezo mbali mbali katika kambi za wakimbizi nchini. Waziri Murkomen alisema hayo katika hafla ya kuwatuza watengenezaji wa filamu kutoka kambi za wakimbizi zilizoko nchini. Kuanzishwa kwa michezo katika kambi za wakimbizi, kulingana na Murkomen ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuwahamasisha wakimbizi katika jamii ya Kenya.
Ligi kuu ya Uingereza kutinga raundi ya 6 wikendi hii
Ligi kuu ya Uingereza maarufu kama EPL inaingia raundi ya sita ya msimu 2024/2025 wikendi ya tarehe 28 na 29 mtawalia kwa jumla ya mechi tisa. Jumamosi 28, Newcastle itakuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester City watakaokosa kiungo cha kati Rodri katika mechi ya mapema mwendo wa saa nane na nusu adhuhuri. Siku hiyo, mwendo wa saa kumi na moja jioni jumla ya michuano tano itagaragazwa katika viwanja mbali mbali.
Maafisa 7 wa KPLC wana kesi ya kujibu, mahakama yaamua
Mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi ya Milimani imewapata washukiwa 7 wa ufisadi na kesi ya kujibu iliyowasilishwa na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma (ODPP) kortini humo. Mahakama hiyo mnamo Alhamisi 26, iliwapata wafanyakazi 7 wakuu wa kampuni ya kusambaza nguvu za umeme nchini KPLC na kesi ya kujibu inayohusisha uhalifu wa kiuchumi wa shilingi milioni 150. Saba hao watatakiwa kudhibitishia mahakama kuwa hawana hatia katika kesi wanaohusishwa nayo kutoka kwa ODPP.
Discover how simple it is to make a flower bouquet
• Guide on how you can arrange flowers for a bouquet As a man are you struggling to get your girlfriend a stunning bouquet despite her requests? Buying a pre-made arrangement can be costly, especially when you adore flowers. Worry less! discover how to craft your own beautiful bouquets from now on! During the launch of Baileys Strawberries & Cream, the Mpasho team among the guests was thrilled to learn the art of crafting a beautiful bouquet.
How detox smoothies can promote a healthy lifestyle
Detox smoothies have become popular in recent years as a quick, nutritious way to reset your body and boost your health. These vibrant, nutrient-packed drinks promise to flush toxins, improve digestion, and give you a natural energy boost. Whether you're looking for a simple cleanse or want to incorporate more fruits and vegetables into your diet, detox smoothies are an easy, effective option. What is a Detox Smoothie?
How to Thrive in the Gig Economy: Strategies for Success
How to Thrive in the Gig Economy: Strategies for Success The gig economy has exploded in recent years, offering people flexible work opportunities through freelancing, contract jobs, and short-term projects. A gig is a job, especially one that is temporary or freelance and performed on an informal or on-demand basis. While traditional 9-to-5 roles still dominate, the gig economy is reshaping how people approach their careers.
Chuo kikuu cha Karatina chafungwa ghafla
Usimamizi wa chuo kikuu cha Karatina umekifunga ghafla chuo hicho kwa muda usiojulikana. Uamuzi wa kufunga chuo hicho ulitolewa na seneti ya chuo hicho Jumatano mchana baada ya wanafunzi kufanya maandamano nje ya shule hiyo katika eneo la Gitunduti takribani kilomita moja kutoka chuo hicho. Kufuatia kufungwa huko, masomo ya muhula wa kwanza katika mwaka wa masomo 2024/2025 imeahirishwa.
Maafisa 2 wa utunzi wa misitu wakamatwa na EACC kwa madai ulaji rushwa
Wafanyakazi wawili wa idara ya huduma za misitu nchini wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Garissa baada ya kupatikana wakihusika na ulaghai wa pesa za umma. Wawili hao kwa majina Elphas Tembu Wesonga ambaye ni mhifadhi nwa misitu na Ibrahim Aden Hussein anayehudumu katika nafasi ya uhasibu, walikamatwa katika msako uliofanywa na maafisa wa EACC Jumanne tarehe 24.
Mahakama yaruhusu tume ya EACC kumchunguza Kidero
Gavana wa zamani wa kaunti ya Kakamega Evans Kidero amepata pigo baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali ombi lake la kutaka EACC kuwacha kuchunguza akaunti zake za banki. Benchi la majaji watatu lilitupilia mbali ombi la Kidero mnamo Ijumaa tarehe 20. Kidero alishtakiwa na tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC kwa madai ya rushwa, uhalifu wa kiuchumi na kupata mali kwa njia mabzo hakuziweka wazi.
Thailand yaidhinisha ndoa za jinsia moja
Taifa la Thailand limeidhinisha ndoa ya jinsia moja kuwa sheria katika nchi hiyo ikiwa nchi ya kwanza katika ukanda wa kusini mashariki mwa Asia kufanya hivo. Mswada wa kuhalalisha ndoa ya namna hiyo iliwasilishwa katika seneti na kupitishwa mwezi wa Juni. Mfalme Maha Vajiralongkorn alitia sahihi kwa mswada huo utaoanza kutekelezwa Januari 22, mwaka ujao.
CCTV footage shows how Cleophas Malala's son & brother-in-law were kidnapped
UDA secretary general Cleophas Malala Former UDA Secretary General has revealed that his son and nephew were allegedly kidnapped and tortured for 6 hours. He took to his socials announcing that the duo was tortured to share details of Malala's whereabouts and that of his wife. Through his X account, Malala captioned "My Son & my 19-year-old brother-in-law were abducted at gunpoint. Tortured for 6 hours to disclose my whereabouts or that of my wife and to show them the way to my residence.
Chuo kikuu cha Moi chakabiliwa na uhaba wa kondomu
Kenya yakabiliwa na uhaba wa kondomu Chuo kikuu cha Moi jijini Eldoret kimewaonya wanafunzi wake kuwa kuna uhaba wa mipira ya kondomu katika chuo hicho. Kupitia taarifa kwa wanafunzi kutoka kwa idara ya chuo cha sayansi ya afya chuo hicho kimeelezea kuwa kinakumbwa na uhaba mkubwa wa kondomu. Taarifa hiyo ilitiwa sahihi na afisa wa afya ya umma P.I Sekenkei mnamo tarehe 19, Septemba iliwaonya wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho.
Linet Toto's husband confirms the birth of their daughter
Nifty Kim, husband to Bomet Woman Representative Linet Toto has confirmed the birth of their child. He also revealed the gender of the baby while celebrating his wife's birthday. Linet is a mother to a baby girl. Taking to his socials, he captioned "Linet Chepkorir Toto, You are my bosom friend, my privado, my soulmate, and a mother to my beautiful princess. You are turning a year older but to me age doesn't define my love and moments that I will live to cherish with you, forever I will do....
Mhubiri akiri kuweka kamera za siri katika bafu ya kanisa
Polisi wa Michigan wanamzuilia mhubiri mmoja kwa jina Will Johnson kwa kuweka kamera za siri katika bafu la kanisa alilokuwa akihubiri. Polisi wamemfungilia mashtaka mhubiri huyo wa zamani wa kanisa la Jumuiya la 2|42 ambaye alikiri kuweka kamera hizo ili kuangalia watu fulani. Mhubiri Will Johnson ameshtakiwa kwa makosa ya kumchunguza mtu ambaye hajavaa nguo, kuharibu ushahidi na kutumia tarakilishi kutekeleza uhalifu.
Huddah Monroe amwomba radhi Peter Salasya
Mwanashoshalaiti Huddah Monroe ameomba radhi kwa mbunge wa Mumias mashariki Peter Salasya baada ya majibizano makali katika mtandao wa Instagram, Huddah amesema kuwa bado ana heshima na mapenzi ya dhati kwa mheshimiwa huyo anayehudumu muhula wake wa kwanza katika bunge la kitaifa. "Nakuheshimu sana Peter Salasya na naomba radhi kwa kukushambulia . Tuonane hapo juu, Ubarikiwe." Aliandika Huddah Monroe. Awali mbunge Salasya alikuwa amemjibu mwanashoshalaiti huyo kutokana na mashambulizi yake kwake.
NACADA yatoa onyo kwa watayarishaji wa maudhui ya mtandaoni
Mamlaka ya kitaifa ya kupambana na pombe na matumizi ya dawa za kulevya NACADA, imewaonya watengenezaji wa maudhui ya mtandaoni na washawishi dhidi ya kukuza matumizi ya vileo na dawa za kulevya. Hii ni kupitia kwa barua kwa watengenezaji wa maudhui iliyotiwa sahihi na afisa mkuu mtendaji wa NACADA Dkt. Anthony Omerikwa Jumatatu 23, Septemba.
Mwanawe Zinedine Zidane astaafu soka akiwa na umri wa miaka 29
Kifungua mimba wa mwanasoka nguli duniani Zinedine Zidane ametangaza kustaafu kucheza kandanda kitaaluma akiwa na umri wa miaka 29 pekee. Enzo Zidane, amekuwa na wakati mgumu katika taaluma akijaribu kupata nafasi ya kucheza katika ligi kuu za barani Ulaya. Zidane ,29, akitangaza kustaafu kwake kwa wanahabari, amesema kuwa kushinda taji kama vile la michuano ya Ulaya hudhibitisha mtu kuwa mchezaji na anafurahia mambo aliyoweza kufanikisha wakati akiwa mchezaji.
Kocha wa AFC Leopards alalamikia hali mbovu ya uwanja wa Thika
Kocha wa klabu ya AFC Leopards Tomas Trucha amelalamikia hali mbovu ya uwanja wa Thika ambao unatumika katika soka. Malalamishi ya kocha Trucha yanajiri baada ya mechi ya AFC Leopards ugani humo mnamo Jumamosi 21 dhidi ya Bidco United ambapo walishinda mchuano huo kwa bao moja. Picha zilisambaa mtandaoni za wachezaji wa AFC Leopards wakivalia jezi zao katika sehemu wazi kwani uwanja huo hauna chumba maalum cha wachezaji kubadilishia mavazi yao.
Aliyekuwa katibu mkuu wa UDA Cleophas Malala adai mtoto wake alikuwa ametekwa nyara
Aliyekuwa seneta wa kaunti ya Kakamega Cleophas Malala, amedai kuwa mtoto wake na shemeji wake wa miaka 19 walitekwa nyara na baadaye kuachiliwa. Kupitia ukurasa wa X, seneta huyo wa zamani ameandika kuwa mwanawe na shemeji wake walitekwa nyara kwa mtutu wa bunduki. Malala amekiri kuwa baada ya kutekwa nyara kwa familia yake, waliteswa kwa takribani saa sita, watekaji nyara wakiwataka kuelezea alipo ama mke wake.
Kasmuel McOure aomba msamaha kwa kukutana na MP Osoro
Mwanaharakati Kasmuel McOure ameomba radhi wafuasi wake kwa kuonekana akicheka na mbunge Silvanus Osoro katika picha na video iliyosambaa mtandaoni. McOure amesema kwamba anajutia kukubali kupiga picha na mjumbe. Kasmuel amesema kuwa amepokea jumbe nyingi kwenye simu yake kutoka kwa watu mbali mbali wanaomfuatilia wakimtaka kuweka wazi ikiwa amejiunga na serikali. "Sijafanya kazi na serikali, nimepata ofa mara nyingi na nimefikiwa mara nyingi tangu tulipoanza maandamano." Alisema Kasmuel.
Washukiwa wa utekaji nyara wa mwanablogu Chawa-001 wafikishwa mahakamani
Kesi dhidi ya washukiwa wa utekaji nyara wa mwanablogu Bruce John Kajira maarufu kama Chawa 001, walifikishwa katika mahakama ya Shanzu kujibu mashataka dhidi yao mnamo Jumatatu 23, Septemba. Washukiwa hao wanne waliotambulika kama Abdul Hassan Athman, Esther Muthoni,Violet Adera na Haji Babu Ndau Mohamed walikana mashtaka dhidi yao mbele ya mahakama ya sheria namba 4 ya Shanzu.
Faith Kipyegon na Beatrice Chebet watambuliwa na shirika la kielimu nchini Marekani
Wanariadha wa Kenya Faith Kipyegon na Beatrice Chebet wamepokezwa tuzo ya kifahari na shirika la kielimu la Chuo cha Mafanikio cha Marekanini katika hafla iliyoshuhudiwa na rais William Ruto katika jumba la Lincoln Centre Plaza jijini New York. Chuo cha Mafanikio cha Marekani kinachojulikana kama Academy of Achievements ni shirika la elimu lisilo la faida ambalo linatambua baadhi ya watu wanaofaulu zaidi duniani katika nyanja mbalimbali na kuwapa fursa ya kukutana.
Bodi ya uchaguzi wa FKF yazinduliwa jijini Nairobi
Bodi itakayosimamia uchaguzi wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF imezinduliwa katika hafla iliyoandaliwa hotelini Kempinski jijini Nairobi. Bodi hiyo yenye wanachama watano imetwikwa jukumu la kusimamia uchaguzi wa utawala mpya wa FKF kwa miaka minne ijayo .Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika hivi karibuni. FKF imekuwa chini ya rais Nick Mwendwa ambaye amehudumu kwa zaidi ya miaka minane katika awamu mbili.
Gavana wa Nandi awafuta wafanyakazi 1,800 wa kaunti
Gavana wa kaunti ya Nandi Stephen Sang amewafuta kazi wafanyakazi wapatao 1,800 waliopata nafasi za kazi katika sekta mbali mbali kwenye kaunti hiyo kuanzia mwaka wa 2013. Akizungumza na wanahabari mapema Jumatatu, gavana Sang alisema kuwa hatua hiyo inajiri baada ya ushauri kutoka kwa ripoti ya ukaguzi wa rasilimali watu ya kaunti hiyo. Gavana Sang amesema kuwa atatekeleza ushauri wote kwa asilimia mia kutoka kwa ripoti iliyowasilishwa kwake.
Magavana wa zamani kuhukumiwa mahakamani wiki hii
Waliokuwa magavana Mike Sonko wa Nairobi na Mwangi wa Iria wa Murang'a watahukumiwa katika mahakama ya kupambana na ufisadi ya Milimani jijini Nairobi tarehe 25 na 36 Septemba mtawalia. Tume ya maadili na kupambana na rushwa EACC iliwashtaki wawili hao kwa madai ya kuvuja rasilimali za umma kwa minajili ya kujifaidisha. Mike Mbuvi Kioko Sonko maarufu kama Mike Sonko alishtakiwa pamoja na wengine watatu kwa madai ya kupeana zabuni kinyume cha sheria.
Wawili wakamatwa na bangi ya thamani ya milioni 9.4
Maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha kupambana na dawa za kulevya katika kaunti ya Kwale wamewakamata watu wawili na bangi ya thamani ya shilingi 9,241,500. Wawili hao wamekamatwa kufuatia msako wa maafisa wapolisi katika eneo la Kona ya Chief, Diani kaunti ya Kwale. Maafisa wa kupambana na dawa za kulevya walipokea taarifa kuhusu walanguzi hao wawili.
"Mimi sio kienyeji!" Huddah amjibu Salasya baada ya kutangaza amechoka kujaribu kumtongoza
Mwanasosholaiti wa Kenya Huddah Monroe amemjibu mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya akimbainisha kuwa yeye sio kienyeji. Awali mbunge Salasya alisema kuwa amekata tamaa kuendelea kujaribu kumtongoza Huddah. Salasya alisema kuwa hawezani na Huddah akidai kwamba serikali itaanguka. "Mimi siwezani wataangusha serikali afadhali nirudi kwa vienyeji yangu. Najitenga rasmi kumfuata huyo msichana," Alisema Salasya.
CHADEMA yakiri Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu amekamatwa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA cha Tanzania kimeripoti kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu amekamatwa na jeshi la polisi. CHADEMA imeripoti hayo mapema asubuhi ya Jumatatu ikiarifu kuwa jeshi la polisi halikutoa taarifa ya ni kituo kipi cha polisi kiongozi huyo wa chama cha upinzani nchini Tanzania anazuiliwa. Kupitia ukurasa wa X, CHADEMA imeandika kuwa Lissu alikamatwa nyumbani kwake eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam na kuchukuliwa na msafara wa magari kumi na moja.
Bayern Munich watesa katika ufungaji magoli
Kocha Vincent Kompany anazidi kuendeleza msururu wa kushinda mechi kwa mabao mengi na timu ya Bayern Munich. Bayern Munich imefunga mabao ishirini katika mechi tatu mfululizo ndani ya siku saba; moja ya klabu bingwa barani Ulaya na mbili za ligi kuu Ujerumani - Bundesliga. Mnamo tarehe 14 Septemba, Bayern waliwacharaza Holstein Kiel mabao sita kwa moja katika ligi ya Bundesliga.
Zaidi ya Wakenya 1,800 wanafanya kazi katika makao makuu ya UN
Rais William Ruto amejivunia kuwa kuna zaidi ya raia elfu moja na mia nane wa Kenya wanaofanya kazi katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa UN jijini New York, Marekani. Katika safari ya rais nchini Marekani kushiriki mkutano mkuu wa umoja wa mataifa wa 79 maarufu kama UNGA79, rais Ruto alikutana na Wakenya wanaoishi Marekani na ambao ni wafanyakazi wa umoja wa mataifa. Rais Ruto alikutana na Wakenya hao katika afisi za utume wa kudumu wa Kenya jijini New York.
Jina la uwanja wa Kirigiti kubadilishwa, asema waziri Murkomen
Waziri wa maswala ya vijana, sanaa na michezo Kipchumba Murkomen amedokeza kuwa uwanja unaokaribia kukamilika kujengwa wa Kirigiti, utabadilishwa jina. Waziri Murkomen amesema kuwa uwanja huo ni wa kihistoria tangu jadi za ukoloni kwani rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta alihutubia umaa kwa mara ya mwisho kabla ya kukamatwa na kuzuiliwa katika gereza la Lokiatang. Uwanja huo baada ya kukamilika, waziri Murkomen amedokeza kuwa jina lake litabadilishwa na kuitwa 'Freedom Stadium'.
Watu wanne wauawa katika kisa cha kufyatuliwa risasi Marekani
Watu wanne wamefariki na idadi ya watu wengine ambayo haijawekwa wazi wamepata majeraha katika kisa ambapo watu wasiojulikana waliwafyatulia raia marisasi. Kisa hicho kilitukia siku ya Jumamosi jioni katika eneo la Birmingham, jimbo la Alabama nchini Marekani. Afisa wa police kwa jina Truman Fitzgerald alisema kuwa idadi ya watu isiyojulikana na ambao walikuwa wamejihami kwa bunduki walifyatua marisasi kwa kundi la watu na kuua watu wanne na kujeruhi wengine kadhaa.
Auntie Jemimah asema kuwa anaogopa mapenzi
Mchekeshaji maarufu Auntie Jemimah amesema kuwa hajaweka maswala ya ndoa kama kitu chenye kipaombele katika maisha yake. Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha habari cha mtandaoni, Auntie Jemimah amesema kuwa anaogopa ndoa sana. Aidha, licha ya kuwa ameona ndoa zilizonawiri, kwake binafsi hajaweka maswala ya kuingia katika ndoa kamaswala muhimu sana linalohitaji kuwekwa kipaombele. "Ndoa huwa si kitu cha kipaombele, naogopa ndoa sana." Alisema Auntie Jemimah.
Gen Muhoozi- No civilian will rule Uganda after Mugabe
Museveni's son General Muhoozi has left many upset after stating no civilian would ever rule Uganda after his dad exits the Presidency. In a now-deleted tweet, Muhoozi posted "No civilian will lead Uganda after resident Museveni. The security forces will not allow it. The next leader will be a soldier or a policeman He went ahead to deny that he wouldn't vie for a political seat in 2026 further asking people to support Museveni's on his quest to vie for Presidency for the 7th time.
Gen Muhoozi- No civilian will rule Uganda after Museveni
Museveni's son General Muhoozi has left many upset after stating no civilian would ever rule Uganda after his dad exits the Presidency. In a now-deleted tweet, Muhoozi posted "No civilian will lead Uganda after resident Museveni. The security forces will not allow it. The next leader will be a soldier or a policeman He went ahead to deny that he wouldn't vie for a political seat in 2026 further asking people to support Museveni's on his quest to vie for Presidency for the 7th time.
Gor Mahia na Police FC waaga mashindano ya bara Afrika
Vilabu vya kabumbu kutoka Kenya Gor Mahia na Kenya Police FC vimeaga mashindano ya shirikisho ya soka Afrika CAF. Kenya Police FC iliaga mashindano ya mashirikisho ya Afrika siku ya Ijumaa 20, Septemba baada ya kupoteza mechi ya mkondo wa pili kwa kushindwa kwa mabao 2 kwa moja. Mkondo wa kwanza katika mechi iliyochezewa ugani Kasarasni,Zamaleck ya Misri iliilaza Police FC bao moja kwa nunge kwa hivyo kuongeza matumaini ya kuendelea hatua za mbele kutokana na bao la ugenini.
Shule ya St. Monica Kitale yafungwa ghafla
Shule ya upili ya wasichana ya St. Monica Kitale katika kaunti ya Trans Nzoia imefungwa ghafla baada ya wanafunzi kuandamana wakimtaka mwalimu mkuu wa shule hiyo kuhamishwa. Maandamano hayo ya wanafunzi ya Jumapili asubuhi yawefanywa wanafunzi wakilalamikia usimamizi mbaya wa shule kutoka kwa mwalimu mkuu Bi. Grace Anyango. Inaripotiwa kuwa baadhi ya wanafunzi wamelalamikia maswali mengi wanayokumbana nayo shuleni humo.
Mwakilishi wadi maalum Ezra Kabuga Kihara aaga dunia kupitia ajali
Mwakilisji wadi maalum katika bunge la kaunti la Kiambu Ezra Kabuga Kihara ameaga dunia katika ajali ya barabarani mapema Jumapili tarehe 22 Septemba katika barabara ya Thika karibu ya shule ya upili ya Mangu. Kifo cha MCA Ezra kimedhibitishwa na gavana wa kaunti ya Kiambu mheshimiwa Kimani Wamatangi kupitia timu yake ys mawasiliano.
Polisi wa Kenya nchini Haiti wadai kucheleweshwa kwa vifaa wanavyohitaji
Maafisa wa polisi wa Kenya wanaondeleza urejesho wa amani na utulivu katika nchi ya Haiti wamelalamikia kuhusu maswala kadhaa wanayokumbana nayo katika opreseheni yao nchini humo. Katika kikao cha pamoja baina ya rais William Ruto na polisi hao,rais Ruto alitaka kufahamu matatizo wanayopitia maafisa hao wakati wa wa operesheni zao' Afisa mmoja alisema kuwa kuna chnagamoto nyingi wanapitia kazini ikiwemo kucheleweshwa kwa silaha wanazohitaji katika kupambana na magenge hatari ya Haiti.
Ni kuhusu 2027, Hakuna kingine, akiri Kimani Ichung'wah
Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Kimani Ichung'wah amekiri kuwa joto la kisiasa linaloendelea kwa sasa nchini ni kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Kupitia mtandao wako wa X, mbunge Ichung'wah amesema kuwa matukio yanayoshuhudiwa kisiasa nchini ni kuhusu urithi wa uongozi.
Rais Ruto atembelea kikosi cha polisi cha Kenya nchini Haiti
Rais Dkt. William Ruto Jumamosi alitembelea kikosi cha polisi wa Kenya waliotumwa nchini Haiti kuisaidia nchi hiyo kurejesha amani baada ya kushuhudiwa utovu wa usalama kutoka kwa magenge ya uhalifu wa ndani ya nchi hiyo. Kenya ilituma jumla ya polisi elfu moja nchini Haiti katika mpango wa baraza la usalama la umoja wa mataifa UNSC kama sehemu ya ujumbe wa msaada wa usalama wa kimataifa maarufu kama MSS kurejesha utulivu nchini humo. Rais Dkt.
Stevo Simple Boy asusia safari ya Saudi Arabia
Msanii Stevo Simple Boy ametishia kupangua tumbuizo aliloandaliwa nchini Saudi Arabia kwa kutumiwa tiketi ya ndege ya daraja la watu wa kawaida yaani economy class badala ya daraja la watu wa biashara. Kulingana na mkala wa Stevo, safari ya kuelekea Saudi Arabia ilifaa kufanyika tarehe 22 lakini alisikitikia kuwa safari hiyo huenda ikakosa kufanyika.
Bunduki yanaswa kutoka mikononi mwa majambazi
Polisi katika kaunti ya Garissa wanawazulia watu watatu wanaoaminika kuwa wezi wa kimabavu ambao wamekuwa wakiwahaingaisha wananchi katika eneo la Burburis. Polisi wa utawala kwa ushirikiano na maafisa kutoka idara ya upelelezi DCI na polisi wa kawaida waliwakamata watatu hao katika operesheni ya kijajusi. Washukiwa wawili kwa jina Isaac Muhumed maarufu kama Jografia wa umri wa miaka 38 na mwenzake Muhumed Bare Hussein wa miaka 30 walikamatwa katika sehemu yao ya maficho.
Show More
loading
Actions
Is this you?
As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.Get in touch with Brandon
Contact Brandon, search articles and posts on X, monitor coverage, and track replies from one place.
Learn more about Muck Rack