Muktasari: Mchezo huo unasuburiwa kwa hamu na mashabiki wengi kuona kama KIUT yenye historia ya kufunga vigogo wa ligi, baada ya kuzifunga JKT kwa pointi 84-74 na UDSM Outsiders 68-58 kama itaweza kuizuia Dar City. ULE uhondo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) unatarajiwa kurejea upya kesho Ijumaa na Uwanja wa Donbosco Upanga kutakuwa na vita nzito kati ya Dar City dhidi ya KIUT.
Is this you? As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.
Claim your profile
Articles by Brown Msyani
Bahati Mgunda apeleka ujuzi Namibia
Muktasari: Mgunda alichaguliwa na Fiba Afrika kuwa mkufunzi kutokana na mafunzo ya siku tano yaliyofanyika nchini yalishirikisha watoto 85 na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa makocha kutoka Afrika. KOCHA mkongwe wa mpira wa kikapu, Bahati Mgunda ni miongoni mwa makocha 17 wanaotarajiwa kutoa mafunzo kwa watoto nchini Namibia, yalijulikanayo kama Min Basketball yatakayofanyika Uwanja wa Shule ya Augustinium.
Jesca avunja rekodi ufungaji
Muktasari: Hata hivyo, katika mashindano Taifa alifunga pointi 90 peke yake kati ya 172-58 walizoifunga Dodoma, huku mchezo mwingine aliofunga pointi nyingi ulikuwa dhidi ya Pwani aliotupia 56 ambao Dar ilishinda 108-43. Mchezaji wa JKT Stars na timu ya wanawake ya Mkoa wa Dar es Salaam, Jesca Ngisaise amevunja rekodi ya kufunga pointi nyingi peke yake, ambapo alivuka kiwango kilichozoweleka cha pointi zisizozidi 50 kwa mchezo ambacho mastaa wengi hufikia.
BDL ilihamia Taifa Cup
Muktasari: Mara iliwakilishwa na mastaa kama Baraka Sabibi, Mussa Chacha wanaokipiga JKT ilhali Abass Omary, Mwinyi Pembe, Jonas Mushi, Evance Davies na Tyrone Edward wanaichezea Stein Warriors. Ushindani wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ulihamia katika fainali ya mashindano ya Kombe la Taifa kati ya Dar es Salaam na Mara, ambapo ulitokana na ubora wachezaji wa timu zote mbili kutokana na jinsi walivyozoeana wakutanapo kwenye BDL.
Wanafunzi walioduwaza wakongwe kikapu taifa
Muktasari: Hicho ndicho ilichofanya timu ya kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (Dream Team) wanaume na ile ya wanawake ya Mkoa wa Arusha katika mashindano ya Kombe la Taifa yaliyomalizika mjini Dodoma. KAMA una malengo ya kufanya vizuri katika mashindano cha kwanza unatakiwa ufanye maandalizi ya kutosha na uwe na wachezaji wenye uwezo mkubwa.
Vita ya BDL kurudi Julai 10
Muktasari: Ratiba iliyotolewa na kamishina wa ufundi na mashindano wa BDL, Haleluya Kavalambi, imeonyesha mchezo wa kwan-za utakuwa kati ya Kurasini Divas na DB Troncatti, ukifuatiwa na mchezo kati ya Pazi Queens na Reel Dream. BAADA ya kukosa kuangalia utamu wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kwa wiki mbili, ligi hiyo itaendelea tena Julai 10, kwenye Uwanja wa Donbosco, Upanga.
Mushi mzuka mwingi ufungaji pointi kikapu
Muktasari: Mushi aliyewahi kuwa mfungaji bora katika mashindano ya kanda ya tano ya Afrika, ameshika nafasi hiyo baada ya kufunga pointi 128. BAADA ya Jonas Mushi kutoka timu ya Stein Warriors kushika nafasi sita katika ufungaji wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ametamba kurudi katika nafasi yake ya kwanza aliyoizoea. Mushi aliyewahi kuwa mfungaji bora katika mashindano ya kanda ya tano ya Afrika, ameshika nafasi hiyo baada ya kufunga pointi 128.
Ligi Shinyanga inaanza upyaaa
LIGI ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Shinyanga inatarajia kuendelea Jumapili, kwa mchezo kati ya timu ya B4 Mwadui na Risasi. Mchezo huo wa Ligi ya Mkoa, utafanyika kwenye Uwanja wa Risasi. Kamishna wa ufundi na mashindano wa Ligi hiyo George Simba, amesema Ligi ya mkoa huo ilisimama kupisha mashindano ya Kombe la Taifa. Alisema Ligi itaendelea tena kesho (Jumatatu) kwenye Uwanja wa Kahama kwa mchezo kati ya timu ya Kahama Six-ers na Veta.
Tausi yawatia hofu vigogo
Muktasari: Kasi ya Tausi Royals imezishtua timu zingine zinazoifuatia, huku zikionekana kutoa sapoti kwa timu zinazocheza nayo. Kama hujui Tausi Royals imewekwa mtu kati na timu tatu zinazoifuatia katika msimamo wa Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa wanawake (WBDL) ikiwa inashiriki kwa mara ya pili na mara hii hadi sasa inaongoza katika msimamo ikiwa na pointi 14. Timu zingine zenye pointi 14 ni Jeshi Stars, JKT Stars na DB Troncatti.
City Bulls yageuka shamba la bibi
Muktasari: Hali hiyo imeifanya timu hiyo ishindwe kuonyesha makali katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), kama ilivyozoeleka miaka mingi nyuma. TIMU ya kikapu ya Vijana maarufu kama City Bulls imegeuka kuwa sehemu ambayo wachezaji wake wanachukuliwa bila na timu zingine hivyo kuwa sawa na akademi inayoibua wanamichezo na kisha wanaondoka. Hali hiyo imeifanya timu hiyo ishindwe kuonyesha makali katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), kama ilivyozoeleka miaka mingi nyuma.
Kilichowaponza JKT, UDSM DBL ni hiki hapa
Muktasari: Ligi hiyo ambayo kwa sasa imesimama kupisha mashindano ya Kombe la Taifa, imekuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka iliyopita. Kujiamini kwa JKT na UDSM Outsiders, ndiko kulikofanya hadi timu hizo zikapoteza michezo yao miwili ya Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL). Ligi hiyo ambayo kwa sasa imesimama kupisha mashindano ya Kombe la Taifa, imekuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka iliyopita.
Dar City wanatupia tu BDL
Muktasari: Dar City imefunga pointi hizo, kutokana na michezo nane, ikiongoza pia katika msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 16. Dar City inaongoza kwa kufunga pointi 756, katika Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL). Dar City imefunga pointi hizo, kutokana na michezo nane, ikiongoza pia katika msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 16. Inayofuatia ni Savio iliyofunga pointi 654, Stein Warriors 594, JKT 580, KIUT 538, Srelio 523, Kurasini Heat 497, ABC 493 na Vijana ‘City Bulls’ 492.
Makocha wapewa akili Taifa Cup
Muktasari: Kibonajoro aliyasema hayo kutokana na kasumba iliyokuwepo ya viongozi wa mkoa, kutegemea wachezaji kutoka Mkoa wa Dar es Salaam. Katibu mkuu wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Kigoma Anasi Kibonajoro ameishauri mikoa iwe inatumia wachezaji wake katika mashindano ya Taifa Cup. Kibonajoro aliyasema hayo kutokana na kasumba iliyokuwepo ya viongozi wa mkoa, kutegemea wachezaji kutoka Mkoa wa Dar es Salaam.
29 wa kigeni wakoleza utamu BDL
Muktasari: Idadi ya nyota hao imekuwa ikiongezeka na wamesajiliwa katika timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo na waliopo hadi sasa ni 29. USHINDANI na uwepo wa nyota wa kigeni katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), umeifanya izidi kuimarika na kuwa moja ya zinazoongoza kwa ubora Ukanda wa Afrika Mashariki. Idadi ya nyota hao imekuwa ikiongezeka na wamesajiliwa katika timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo na waliopo hadi sasa ni 29.
Tausi Royals haishikiki WBDL
Muktasari: Huu ni mwaka wa pili kwa timu hiyo kushiriki ligi hiyo na imeongoza kwa kufunga pointi 666 katika michezo saba iliyocheza, huku JKT Stars ikifunga pointi 563. Tausi Royals haishikiki katika Ligi ya kikapu Dar es Salaam (WBDL) na inaongoza kwenye msimamo ikiwa na pointi 14 ikifuatiwa na JKT Stars yenye 13. Huu ni mwaka wa pili kwa timu hiyo kushiriki ligi hiyo na imeongoza kwa kufunga pointi 666 katika michezo saba iliyocheza, huku JKT Stars ikifunga pointi 563.
JKT, UDSM Outsiders mambo magumu Dar
Muktasari: Ubabe wa timu kongwe za JKT na UDSM Outsiders pamoja na Srelio na Savio ulijikuta ukielea kufuatia vipigo visivyotarajiwa kutoka kwa timu hizo ambazo zinachukuliwa kuwa changa katika mashindano hayo. TIMU za kikapu ya KIUT na DB Oratory zimezitikisa timu kongwe zinazoshiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) baada ya kuzifumua katika mechi zilizokutana wiki hii.
Wakongwe watikisika BDL
Muktasari: KIUT ilionyesha ubabe wake kwa kuichapa JKT kwa pointi 84-74, kisha kuifunga UDSM Outsiders kwa pointi 64-53 na kocha wa timu hiyo, Denisi Funganoti alisema mipango waliyojiwekea ya kufanya vizuri katika michuano hii ndiyo chachu ya ushindi. KIUT na DB Oratory zimeendelea kuzitikisa timu kongwe zinazoshiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kutokana na kutokuzihofia na kuzitembezea vichapo.
Noela, Juliana wachuana kwa asisti
Muktasari: Noela ambaye msimu uliopita aliichezea Vijana Queens, msimu huu ameonyesha kiwango kizuri akiwa na Jeshi Stars, huku Juliana Sambwe wa Tausi Royals anayecheza nafasi ya namba 1 (Pointi Guard) ni pili akiwa na asisti 31. WAKATI ushindani kwa timu za wanawake ukizidi kushika kasi katika Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (WBDL), kwa upande wa asisti, Noela Uwendameno kutoka Jeshi Stars anaongoza kwa kutoa 34.
Srelio yainyoosha Mgulani JKT
Muktasari: Tambo za kocha huyo zimekuja baada ya kuwepo na muunganiko mzuri wa wachezaji wake kwa sasa, tofauti ilivyokuwa katika michezo yao ya mwanzo. BAADA ya Srelio kuifunga Mgulani JKT kwa pointi 107-64, kocha wa timu hiyo Miyasi Nyamoko amesema ushindi huo umewanyooshea njia ya kucheza hatua ya nane bora. Tambo za kocha huyo zimekuja baada ya kuwepo na muunganiko mzuri wa wachezaji wake kwa sasa, tofauti ilivyokuwa katika michezo yao ya mwanzo.
Jesca afunika kwa kutupia WBDL
Muktasari: Jesca alifunga pointi hizo, wakatiJKT Stars ilipoifunga Mgulani Stars kwa pointi 121-23. NYOTA wa JKT Stars, Jesca Ngisaise amefunika kwa kufunga pointi 62 pekee yake katika mchezo mmoja wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL). Jesca alifunga pointi hizo, wakatiJKT Stars ilipoifunga Mgulani Stars kwa pointi 121-23. Mbali kufungaji pointi hizo, alifunga tena pointi 60 peke yake katika mchezo wao dhidi ya UDSM Queens, JKT Stars ikishinda kwa pointi 109-26.
Nyota Savio aongoza kutupia BDL
Muktasari: Mchezaji huyo amegeuka moto katika mashindano hayo na ubora wake umekuwa ukionekana kila anapokuwa karibu na nyavu, kwani ni nadra kukosa kikapu anaposhuti. WAKATI ushindani wa ufungaji ukiendelea katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), huko kunaonyesha kwamba nyota wa Savio, Ntibomela Bukenge ndiye anayeongoza kwa ufungaji akiwa keshatupia pointi 124.
Kahama Sixers yaivuruga Veta
Muktasari: Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Veta, katika mchezo wa kwanza kwa timu hiyo, Kahama Sixers iliishinda Risasi kwa pointi 54-46. TIMU ya mpira wa kikapu ya Kahama Sixers imedhihirisha ubora ilionayo katika Ligi ya Mkoa wa Shinyanga baada ya kuiadhibu Veta kwa pointi 75-37. Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Veta, katika mchezo wa kwanza kwa timu hiyo, Kahama Sixers iliishinda Risasi kwa pointi 54-46.
ABC yaipokea UDSM Outsiders
Muktasari: Kushuka kwa Outsiders kumeifanya ABC iongoze Ligi hiyo kwa pointi 12, ikifuatiwa na Dar City iliyopata pointi 10. KICHAPO ilichopewa UDSM Outsiders kutoka kwa KIUT cha pointi 65-60, kimeifanya timu hiyo ishuke katika uongozi wa msimamo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) hadi kwenda nafasi ya tano ikiipisha kileleni ABC. Kushuka kwa Outsiders kumeifanya ABC iongoze Ligi hiyo kwa pointi 12, ikifuatiwa na Dar City iliyopata pointi 10.
Timu ya Nahreel yazinduka WBDL
Muktasari: Dream iliyoanzishwa na Emmanuel Mkono ajulikanaye kwa jina la kisanii kama Nahreel, katika mchezo huo iliishinda Kigamboni Queens kwa pointi 78-49 kwenye Uwanja wa DonBosco uliopo Upanga, Dar es Salaam. KAMA utani timu ya mpira wa kikapu ya Real Dream iliyoanza kwa kukatisha tamaa mashabiki katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL), imeshangaza wengi ni baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika mchezo dhidi ya Kigamboni Queens.
Savio yashindwa kuonyesha makali
Muktasari: Savio iliyozoeleka kucheza vizuri katika mzunguko wa pili, katika ligi ya msimu huu inayochezwa mzunguko mmoja, imeonyesha itakuwa na wakati mgumu kufanya vizuri. WAKATI Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ikizidi kushika kasi, mambo bado hayajakaa vizuri kwa timu kongwe ya Savio baada ya kuchemsha katika mechi zake kadha za ligi hiyo.
Kipigo chaishtua Srelio, yafuata mastaa DR Congo
Muktasari: Katika michezo ya awali ya mashindano hayo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Donbosco, Upanga, timu hiyo ilifungwa na Mchenga Star kwa pointi 82-70, Dar City 105-32 kisha ikaifunga Chui kwa pointi 55-52 huku mchezo wa nne ikifungwa na Pazi kwa pointi 81-73. BAADA ya Srelio kufungwa na Pazi kwa pointi 81-73 katika mchezo wa Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (BDL), kocha wa timu hiyo, Miyasi Nyamoko amesema wameamua kuwaita nyota wawili kutoka DR Congo ili waje kuokoa jahazi.
Stein, Dar City patachimbika BDL
Muktasari: Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa kikapu utachezwa saa 2:00 usiku, huku Stein Warriors inayoongoza kuwa na wapenzi wengi katika Ligi ya BDL, inakutana na timu ngumu isiyotabirika ya Dar City. ULE uhondo wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) unaendelea tena leo kwenye Uwanja Donbosco Upanga wakati Stein Warriors na Dar City zitakaposhuka uwanjani kuonyeshana kazi katika mfululizo wa ligi hiyo inayozidi kushika kasi.
Srelio haitaki kurudia makosa
Muktasari: Ligi hiyo ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), itaendelea kesho Jumamosi kwa michezo minane itakayochezwa kwenye Uwanja wa Donbosco Upanga unaotumika. BAADA ya timu ya Srelio kupoteza michezo miwili ya kwanza, kocha wa timu hiyo Miyasi Nyamoko amesema kwa mechi dhidi ya maafande wa ABC hawatarudia makosa katika vita ya Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).
Kahama Sixers yaendeleza moto
Muktasari: Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana fainali ya mwaka jana, Kahama iliishinda Risasi michezo 3-1. KLABU ya Kikapu ya Kahama Sixers imeanza vizuri kampeni ya kutetea taji la ubingwa wa Ligi ya Mkoa wa Shinyanga, baada ya kuifunga Risasi kwa pointi 54-46, katika mchezo uliopigwa kwenye Uuwanja wa Kahama, mjini humo. Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana fainali ya mwaka jana, Kahama iliishinda Risasi michezo 3-1.
Mkosa, Ebongo wawa kivutio BDL
Muktasari: Wachezaji hao wote wanacheza nafasi ya namba 4 “Power Forward” na uwezo wao unafanana na kuwavutia mashabiki wanaohudhuria mechi hizo. WAKATI Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) ikizidi kushika kasi, nyota wa timu mbili tofauti, Amin Mkosa wa Dar City na Mikado Ebengo wa DSM Outsiders wameonekana kuwa kivutio katika Ligi hiyo. Kivutio cha wachezaji hao, imetokana na uwezo wa kucheza vizuri katika nafasi wanazocheza na kuzibeba timu zao.
Mavitu ya Hasheem Thabeet gumzo BDL
Muktasari: Lakini, mbali na ubora wa staa huyo aliyewahi kukipiga katika ile Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) ambako kuna mastaa kama LeBron James, Kelvin Durant, Giannis Antetokounmpo, Luka Doncic na wengineo, unaambiwa mashabiki wanaovijaza viwanja vya Donbosco, Upanga, Dar es Salaam wanamfuatilia zaidi mchezaji huyo.
Kahama Sixers, Risasi vita nzito Shinyanga
Kahama Sixers na Risasi zinatarajiwa kucheza Jumapili mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mkoa wa Shinyanga. Katika fainali ya mwaka jana, Kahama Sixers iliishinda Risasi michezo 2-1 na katika mchezo wa kwanza ilishinda pointi 67-62. mchezo wa pili, Risasi ilishinda kwa pointi 102-100, huku Kahama Sixers ikishinda katika mchezo wa tatu kwa pointi 87-60. Kamishina wa ufundi na mashindano wa ligi ya kikapu wa mkoa wa huo, George Simba alisema mchezo huo wa ufunguzi utachezwa katika Uwanja wa Kahama.
Baada ya Vijana kuifinya Savio UDSM, Stein kazi ipo
Muktasari: Savio iliyowahi kuwa bingwa wa ligi hiyo ya BDL 2015, 2016, 2017, 2018 na 2021, ilishindwa kuonyesha makali yao kama ilivyozoeleka. KIWANGO cha chini kilichoonyeshwa na Savio kilisababisha ifungwe na Vijana ‘City Bulls’ kwa pointi 70-50, katika Ligi ya kikapu Dar es Salaam inayofanyika katika Uwanja wa Donbosco, Upanga. Savio iliyowahi kuwa bingwa wa ligi hiyo ya BDL 2015, 2016, 2017, 2018 na 2021, ilishindwa kuonyesha makali yao kama ilivyozoeleka.
Msimu mpya BDL/WBDL, kazi imeanza DonBosco
Muktasari: Kamishina wa ufundi na mashindano hayo, Haleluya Kavalambi alisema ligi ya mwaka huu itachezwa katika mzunguko mmoja, baada ya hapo timu nane za juu zitacheza hatua ya robo fainali.
UDSM yapiga mkwara, BDL kupingwa viwanja viwili
Muktasari: Katika fainali hiyo JKT iliifumua UDSM katika michezo 3-1 ambapo katika mchezo wa kwanza JKT ilishinda pointi 67-62, ule pili UDSM ikashinda 66-55 ilhali ule wa tatu na wa nne JKT ikishinda kwa pointi 68-58 na 75-50 mtawalia. JOTO la ufunguzi wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kati ya UDSM Outsiders na JKT linazidi kupanda kutokana na kumbukumbu ya ushindani uliotokea katika fainali ya mashindano hayo mwaka jana.
Dar City kuachia kikosi kabla ya Mei 8
Muktasari: Mbwana aliliambia Mwanaspoti, wachezaji wapya na wa zamani walioongezewa mikataba nao watatangazwa siku hiyo. KOCHA Mkuu wa Dar City, Mohamed Mbwana amesema atatangaza kikosi kitakachoshiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), kabla ya kufungwa dirisha la usajili Mei 8. Mbwana aliliambia Mwanaspoti, wachezaji wapya na wa zamani walioongezewa mikataba nao watatangazwa siku hiyo. Hata hivyo, hakutaka kudokeza majina ya wachezaji wapya na kusisitiza yatatangazwa kabla ya tarehe 8.
Dar City si haba Rwanda
Muktasari: Katika mchezo huo Aliou Diarra alifunga pointi 18 akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Axel Mpayo aliyefunga 12. TIMU ya APR ya Rwanda imeifunga Dar City kwa pointi 81-68 katika nusu fainali ya mashindano ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Petit Gymnasium nchini Rwanda. Katika mchezo huo Aliou Diarra alifunga pointi 18 akifuatiwa na mchezaji mwenzake, Axel Mpayo aliyefunga 12.
BDL ni mwendo wa maokoto, ubora
Muktasari: Timu ya Dar City inamilikiwa na Mussa Mzenji, huku Stein Warriors ikiwa mikononi mwa Karabani Karabani na mbali ya kumiliki timu hizo kila moja ina benchi la ufundi lenye uwezo mkubwa wa kuisimamia. WAKATI timu zikitafuta wawekezaji wa kuzisapoti katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), imeonyesha kuwa Dar City na Stein Warriors ndizo pekee zilizopata wawekezaji.
Mambo ya ndani yaendeleza kicheko
Muktasari: Katika mashindano hayo timu tisa zinashiriki zikiwa zimepangwa katika makundi mawili huku la A likiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ujenzi, Maliasili na Singida MC ilhali lile la B lina Tanesco, NSSF, Dodoma Jiji na Uchukuzi. TIMU ya kikapu ya Wizara ya Mambo ya Ndani imeinyoosha Maliasili kwa pointi 113-34 katika mashindano ya Mei Mosi yanayoendelea katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaja mjini Singida.
Srelio yastukia jambo, JKT ikijibu mapigo
Muktasari: Kocha wa timu hiyo, Miyasi Nyamoko amesema klabu yake imejipanga kushusha nyota wake kabla ya ligi hiyo kuanza Mei 10, mwaka huu ili ianze mapema kufanya maandalizi ya mwisho mwisho ikiamini kwamba kwa sasa wanaendelea kujifua huko waliko.
WBDL kitawaka, timu tano kupambana
Muktasari: Mchuano huo unatokana na maandalizi ya timu hizo pamoja na ubora wa wachezaji zilionao. MCHUANO kwa timu za wanawake utakuwa kwa klabu tano kati ya timu 11 zinazoshiriki Ligi ya Kikapu ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL). Mchuano huo unatokana na maandalizi ya timu hizo pamoja na ubora wa wachezaji zilionao. Timu hizo ni Jeshi Stars, Tausi Royals, JKT Stars, Vijana Queens na ile mpya ya The Reel Dream.
Kigoma yaanza kuibua vipaji
Muktasari: Katibu wa chama hicho, AQ Anasi ameliambia Mwanaspoti kuwa mwamko umekuwa mkubwa kwa vijana wanaojifunza kucheza kikapu. CHAMA cha Kikapu Mkoa wa Kigoma kimetamba kuwa na viwanja wanaochipukia katika mchezo huo ambao ni toleo jipya linalotarajiwa kuwa kutisha siku za usoni. Katibu wa chama hicho, AQ Anasi ameliambia Mwanaspoti kuwa mwamko umekuwa mkubwa kwa vijana wanaojifunza kucheza kikapu.
Wakongwe kikapu kazi wanayo BDL
Muktasari: Ligi hiyo imekuwa ikifanyika katika mizunguko miwili kila mwaka, lakini ile ya mwaka huu itafanyika mzunguko mmoja. Ugumu wa timu hizo unatokana na kasumba ziliyojiwekea ya kucheza vizuri katika mzunguko wa pili, huku zingine zikisubiri nyota wao wafike kutoka wanakoishi. WAKATI Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ikitangazwa kuchezwa mzunguko mmoja, huenda baadhi ya timu kongwe mfumo huo ukazifanya ziwe na wakati mgumu mara itakapoanza.
Masika yasimamisha ligi ya kikapu Arusha
Muktasari: Awali, Chama Mpira wa Kikapu Mkoa Arusha (ARBA) kilipanga kukutana na viongozi wa klabu shiriki ili kukubaliana tarehe ya kuanza mashindano hayo baada ya kushindwa kuanza kutokana na mvua zinazonyesha. MVUA za masika zinazoendelea kunyesha mjini Arusha zimeathiri kuanza kwa mashindano ya Ligi ya Kikapu mkoani humo msimu ujao.
Wachezaji wakimbilia Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam
Muktasari: Ubora wa ligi hiyo unatokana na uwezo wa wachezaji wanaocheza pamoja na ushindani wa timu shiriki ambao umefanya kutoka mikoa mingine na nje ya nchi ili kuja kucheza mashindano hayo. LICHA ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kuendeshwa bila kuwa na udhamini, lakini imeonyesha kuwa ndio inayoongoza kwa ubora na kuvutia mastaa kutoka sehemu mbalimbali wanaokuja kuichezea.
Kuna nini Dar City BDL?
Muktasari: Timu hiyo yenye wachezaji wazoefu kutoka ndani na nje ya nchi, inadaiwa kuonyesha kujiamini zaidi kabla ya kuanza kwa msimu. WAKATI timu zikiwa katika maandalizi kwa ajili Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) msimu ujao, Dar City inaweza kushindwa kuonyesha makali kunatokana na kutoaanza mapema mazoezi ya pamoja. Timu hiyo yenye wachezaji wazoefu kutoka ndani na nje ya nchi, inadaiwa kuonyesha kujiamini zaidi kabla ya kuanza kwa msimu.
Mastaa kikapu walivyonogesha Star League Dar
Muktasari: Mashindano hayo ya mastaa yalishirikisha wachezaji nyota kutoka timu zinazoshiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) waliounda timu nane na kuzipa majina ya wachezaji. Kundi A ilikuwa na Miyasi, Nahreel, Mwalimu, Evance huku lile la B lilikuwa na Soud Black, Mkosa, Mngeja na Labani. TIMU ya Soud Black imetwaa ubingwa wa Ramadhan Star League 2025 baada ya kuifunga Miyasi kwa pointi 64-41 katika fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Donbosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Viongozi BDL wahaha kutafuta saini
Muktasari: Wachezaji walionekana kuwa na wakati mgumu ni wachezaji wa Miyasi, Marcus Tshi, Emanuel Mulumba na Dan Mwendela raia wa Congo. Viongozi wa timu zinazoshiriki ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), walikuwa wakipigana vikumbo kusaka saini za wachezaji wapya katika , wakati wa mashindano ya Ramadhani Star Ligi. Wachezaji walionekana kuwa na wakati mgumu ni wachezaji wa Miyasi, Marcus Tshi, Emanuel Mulumba na Dan Mwendela raia wa Congo. Mwanasposti ililokuwepo uwanjani hapo.
Lipiki achafukwa timu yake kuondolewa
Muktasari: Ukonga iliondolewa katika listi kwa bahati mbaya kabla ya kocha huyo kuulizia kwa wahusika na kurejeshwa na kushusha presha mashabiki wa timu hiyo kuhusu ushiriki wao. Kocha wa Ukonga Queens, Denisi Lipiki amesema timu yake itashiriki Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Wanawake (WBDL). Ukonga iliondolewa katika listi kwa bahati mbaya kabla ya kocha huyo kuulizia kwa wahusika na kurejeshwa na kushusha presha mashabiki wa timu hiyo kuhusu ushiriki wao.
BDL usipojipanga utapangwa
Muktasari: Timu hizo ambazo ni Dar City, Chui, Savio, DB Oratory, na KIUT hazijaonekana zikijifua kokote kwa maandalizi ya ligi hiyo na hata nyota wake hawakuwepo kwenye mashindano maalumu ya Ramadhan Star Ligi. TIMU tano za Ligi ya Mpira wa Kikapu Dar es Salaam (BDL), zimeshindwa kuanza mazoezi hadi sasa na kuonekana zitakuwa na wakati mgumu ligi itakapoanza Aprili.
Show More
loading
Actions
Is this you?
As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.Get in touch with Brown
Contact Brown, search articles and posts on X, monitor coverage, and track replies from one place.
Learn more about Muck Rack