Is this you? As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.
Claim your profile
Articles by Devotha Kihwelo
Korea yaikopesha Tanzania Sh441 bilioni kujenga chuo
Muktasari: Mkopo wa Sh441.12 bilioni kutoka Korea utawezesha ujenzi wa Chuo Mahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (DTI) mkoani Dodoma, kitakacholenga kuzalisha wataalamu wa teknolojia za kisasa, kupunguza pengo la ujuzi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini. Dar es Salaam.
Korea yaikopesha Tanzania Sh441 bilioni kujenga chuo cha Tehama
Muktasari: Mkopo wa Sh441.12 bilioni kutoka Korea utawezesha ujenzi wa Chuo Mahiri cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (DTI) mkoani Dodoma, kitakacholenga kuzalisha wataalamu wa teknolojia za kisasa, kupunguza pengo la ujuzi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini. Dar es Salaam.
Polisi yaonya wanaopanga kufanya fujo siku ya hukumu ya Lissu
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu hali ya usalama jijini humo. Muktasari: Jeshi la Polisi Dar es Salaam limesema linafuatilia taarifa za watu wanaodaiwa kuhamasishana kuingia jijini kufanya fujo Novemba 6, siku ambayo Mahakama Kuu inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu. Dar es Salaam.
Polisi wawaonya wanachuo wapya dhidi ya uhalifu, dawa za kulevya
Mkuu wa Kitengo cha Michezo kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Paschal Nkuba, akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dodoma kupitia kampeni ya Ongea na Freshers. Muktasari: Jeshi la Polisi lawataka kujiepusha na uhalifu, dawa za kulevya na ukatili, huku likisisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria na kutoa taarifa za viashiria vya uhalifu Dar es Salaam.
PPRA yaunganisha mifumo kudhibiti mikataba ya Serikali
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba akizungumza kwenye mkutano wa Wahariri na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina uliofanyika jijini Dar es Salaam. Muktasari: Mfumo wa NeST waunganishwa na mfumo wa usimamizi wa mikataba wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, huku makundi maalumu yakieleza jinsi zabuni zilivyoyabadilisha maisha yao kiuchumi. Dar es Salaam.
Gwajima aonya wanaosambaza video za wahitimu mitandaoni
Muktasari: Waziri Dk Dorothy Gwajima amesema amewasilisha vielelezo kwa mawaziri wa kisekta dhidi ya baadhi ya watu wanaosambaza picha na video za wahitimu wa Aboud Jumbe, akionya kuwa wanaweza kukabiliwa na hatua za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto. Dar es Salaam.
Latra yatangaza maboresho njia moya za daladala Dar, Pwani
Muktasari: Latra imetangaza maboresho ya njia za daladala na kuanzisha njia mpya Dar es Salaam na Kibaha, zikiwemo zinazounganisha Mbagala, Mbande, Pugu na Kigamboni. Wasafirishaji wametakiwa kuomba leseni, huku madereva wakitakiwa kuthibitishwa na mamlaka hiyo. Dar es Salaam.
Wahitimu Shule ya Aboud Jumbe wajutia kauli zao, waomba msamaha
Muktasari: Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Aboud Jumbe, Kigamboni, wameomba radhi kufuatia kauli zao zilizosambaa mitandaoni, huku Mkuu wa Wilaya akisisitiza umuhimu wa malezi na matumizi yenye tija ya mitandao ya kijamii. Dar es Salaam. Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Aboud Jumbe, Kigamboni, Dar es Salaam, wameomba radhi kwa walimu, wazazi, Serikali na Watanzania kufuatia kauli zao zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua mjadala.
Video za wahitimu kidato cha nne zawaibua wadau
Muktasari: Katika video zinazosambaa mitandaoni, baadhi ya wanafunzi wameonekana wakichana na kuchoma moto madaftari na sare za shule, huku wasichana wakiahidi kuchukua waume za watu na wavulana wakisema watajikita katika michezo ya kubahatisha. Dar es Salaam. Pengo katika malezi. Hiyo ndiyo tafsiri ya wadau wa elimu na malezi kuhusu vitendo vya baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne kuchana madaftari na sare za shule na kutoa kauli tata baada ya kumaliza kufanya mitihani ya kuhitimu kidato cha nne.
Operesheni za usiku zafichua madereva wasiozingatia weledi
Muktasari: Madereva wanaoendesha bila leseni halali, wanaobeba abiria kupita kiasi na wanaokiuka masharti ya usalama wamebainika katika operesheni za polisi mikoa mbalimbali, huku wadau wakitaka nidhamu na usimamizi madhubuti kuzuia ajali. Dar es Salaam.
Moto wateketeza maduka 20 stendi mpya ya Buza Dar
Muktasari: Maduka 20 kati ya 64 yameteketea kwa moto katika Stendi Mpya ya Buza kwa Mama Kibonge, Temeke, baada ya hitilafu ya umeme inayodaiwa kusababishwa na kuunganisha waya wa mashine ya kusaga juisi ya miwa. Zimamoto imepanga kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu matumizi ya vizimamoto. Dar es Salaam.
Moto wateketeza vibanda 26 soko la Veterinary Dar
Muktasari: Moto uliotokea Soko la Veterinary, Temeke, usiku wa kuamkia Oktoba 24, 2026, umeteketeza vibanda 26 huku wafanyabiashara walioathirika wakiiomba Serikali kuwasaidia kurejesha mitaji na kuimarisha biashara zao. Dar es Salaam. Vibanda 26 kati ya 230 vilivyopo katika Soko la Veterinary, Temeke, vimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Oktoba 24, 2026, huku wafanyabiashara walioathirika wakikabiliwa na hasara baada ya mali zao kuteketea.
Bima ya Afya kwa Wote II kulenga kaya 625,000
Muktasari: Mchengerwa ataka usajili ufike hadi kwa wananchi wa kipato cha chini, atangaza mabalozi wa bima kila wilaya, akisisitiza afya ni haki na si hisani. Mtwara. Serikali imewataka watumishi wa afya, viongozi wa mikoa na wilaya pamoja na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha mpango wa Bima ya Afya kwa Wote unawafikia wananchi wote, ili Mtanzania yeyote asikose huduma za matibabu kwa sababu ya ukosefu wa fedha.
Tanzania yaanzisha kituo cha kuwaandaa vijana wa Afrika kujadili tabianchi
Mtaalamu wa Nishati, Mabadiliko ya tabianchi na usimamizi wa majanga Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Dk Abbas Kitogo akizungumza na washiriki wa mafunzo ya mabadiliko ya tabianchi yanayofanyika jijini Dar es Salaam ambayo yamehudhuriwa na washiriki kutoka nchi tofauti barani Afrika.
Tabasamu: Bingwa wa hesabu anayelilia ufadhili
Muktasari: Lengo lake si kuonyesha uwezo wa kufanya hesabu kwa kichwa kama anavyosifika kwa uwezo huo, bali kutengeneza njia zinazoweza kuwasaidia wanafunzi wanaokwama wanapokutana na maswali yanayohitaji hatua kadhaa kabla ya kupata jibu. Dar es Salaam. Wakati wanafunzi wengi wakihangaika na kanuni za hisabati, Tabasamu Karimu anasema amebuni njia mbadala za kutatua baadhi ya maswali, akilenga kulifanya somo hilo lieleweke kwa urahisi na kuhusishwa zaidi na maisha halisi.
Kidato cha nne kuanza mitihani kesho, Necta yaonya wakuu wa shule
Muktasari: Watahiniwa 667,040 kuanza mtihani kesho, baraza laonya dhidi ya udanganyifu na kuingiliwa kwa majukumu ya wasimamizi. Dar es Salaam. Jumla ya watahiniwa 667,040 wanatarajiwa kuanza mtihani wa kidato cha nne kesho Jumatatu, Oktoba 19, 2026, utakaofanyika hadi Novemba 6, huku Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) likionya dhidi ya udanganyifu na kuingiliwa kwa majukumu ya wasimamizi.
Siku 30 za TCRA kwa nyaya za intaneti, wananchi wataka utekelezaji
Muktasari: Wananchi na viongozi wa mitaa wataka ukaguzi wa mara kwa mara na hatua madhubuti dhidi ya nyaya za intaneti zinazoning’inia hovyo, baada ya TCRA kuzipa kampuni za mawasiliano siku 30 kurekebisha kasoro zilizobainika. Dar es Salaam.
Wataalamu waonya mashindano ya kula, kunywa kupita kiasi
Muktasari: Onyo hilo linatolewa siku moja baada ya taarifa za kifo cha Edward Gabriel, maarufu Champion, aliyedaiwa kufariki dunia Oktoba 15, 2026, eneo la Muyumbwili, Mtaa wa Karume jijini Arusha, baada ya kushiriki mashindano ya kunywa pombe haramu aina ya gongo kwa lengo la kushinda zawadi ya Sh20,000. Dar es Salaam.
Afrika yaungana kukabili magonjwa yanayovuka mipaka
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Afya ya Tume ya Umoja wa Afrika, Dk Adam Isah akizungumza kuhusu mkutano wa Shirikisho la Tiba ya Usafiri la Pan- Afrika (PATMF) na unaambatana na mkutano wa tisa wa kikanda wa Jumuiya ya Kimataifa ya Tiba ya Usafiri (ISTM) unaofanyika jijini Dar es Salaam na kukutanisha nchini mbalimbali za Bara la Afrika na nje ya bara hilo.
Madereva waliofutiwa pointi warejeshwa shule
Muktasari: Imeelezwa kuwa, hatua hiyo inalenga kuhakikisha madereva wanapata elimu itakayowasaidia kubadili tabia na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani. Dar es Salaam. Madereva waliofutiwa pointi kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani wameanza mafunzo na mitihani, hatua inayolenga kuwajengea uelewa na kuwasaidia kubadili mienendo yao kabla ya kukamilika kwa mchakato wa kuamua kuhusu kurejeshewa leseni zao.
Dereva wa IT akamatwa kwa kuendesha akiwa amelewa
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Njombe, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP, Jane Warioba, akiwa kwenye moja ya basi wakati wa ukaguzi uliofanyika Oktoba 13,2026 mkoani humo Muktasari: Polisi wa Usalama Barabarani mikoa ya Njombe na Iringa wamembaini dereva wa gari la IT akiendesha akiwa amelewa, wakati wa operesheni ya pamoja inayolenga kudhibiti makosa yanayosababisha ajali, hasa nyakati za usiku. Dar es Salaam.
Wenye fremu Tandika waingia matatani kwa kuwaficha wafanyabiashara
Baadhi ya wafanyabiashara wa mitumba Tandika wakiwa wamekusanyika baada ya wenzao kukamatwa na kupelekwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam jana Jumanne, Oktoba 13,2026 katika operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wa barabarani na maeneo yasiyoruhusiwa. Muktasari: Wafanyabiashara wa mitumba walalamikia kukamatwa na kutozwa Sh300,000, DC Temeke awaonya wanaowakinga wanaokwepa doria. Dar es Salaam.
Tanesco yatangaza nafasi za kazi 1,099
Muktasari: Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza nafasi za kazi 1,099 kwa niaba ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), zikiwamo za mafundi, wahandisi, wataalamu wa Tehama na madereva. Nafasi nyingi zaidi ni za fundi daraja la II wa umeme ambazo ni 736, zikifuatiwa na mafundi sanifu wa umeme/elektroniki 193 na madereva 100. Mwisho wa kutuma maombi ni Oktoba 26, 2026. Dar es Salaam.
Afya ya wasafiri kuwakutanisha wataalamu wa Afrika Dar
Katibu wa Shirikisho la Tiba ya Usafiri la Pan-Afrika (PATMF), Dk Charles Tarimo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkutano utakao wakutanisha wataalam wa tiba ya usafiri kutoka Afrika na mataifa mengine utakofanyika jijini Dar es salaam Muktasari: Mkutano utajadili kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, athari za mabadiliko ya tabianchi na namna ya kuboresha maandalizi ya kiafya kabla ya safari. Dar es Salaam.
Latra yatetea utaratibu wa mitihani kwa madereva
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini(Latra), Dk Habibu Suluo akizungumza na Umoja wa Madareva wao kuwepo kwa Coaster za Kukodi Dar es Salaam(UMCD) katika mkutano wao uliofanyika jijini hapa. Muktasari: Mamlaka hiyo imesisitiza madereva kuzingatia masharti ya leseni kwa mujibu wa sheria, huku ikiahidi kusikiliza changamoto zao na kuboresha mifumo ya kidijitali. Dar es Salaam.
Polisi: Msisingizie Mungu ajali zinazotokana na uzembe
Muktasari: Imeelezwa kuwa, changamoto zinazowakabili madereva ni mifumo ya utoaji faini, vidhibiti mwendo (VTS), mabadiliko ya leseni na kufungiwa leseni. Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limewataka madereva kuacha kuhusisha ajali za barabarani na mapenzi ya Mungu, likisema nyingi husababishwa na makosa ya kibinadamu yanayoweza kuzuilika kwa kuzingatia sheria na kuchukua tahadhari.
Yanga njia panda Abuya kurejea dimbani
Kiungo wa Yanga, Duke Abuya. Picha na Mtandao Muktasari: Abuya aliumia katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufanyiwa faulo na winga wa Simba, Libase Gueye. Pamoja na kupatiwa matibabu, kiungo huyo alijaribu kuendelea kucheza kabla ya kushindwa kuendelea dakika ya 25, hali iliyolazimu benchi la ufundi la Yanga kumtoa na kumuingiza Fredy Ngoma.
Yanga njia panda Abuya kurejea dimbani
Kiungo wa Yanga, Duke Abuya. Picha na Mtandao Dar es Salaam. Kiungo wa Yanga, Duke Abuya, anakabiliwa na uwezekano wa kukaa nje ya uwanja kwa muda usiojulikana baada ya kuthibitishwa kupata jeraha la nyama za paja katika mchezo dhidi ya Simba, uliomalizika kwa Yanga kupoteza kwa mabao 2-1.
Ajali barabarani ni zaidi ya uzembe
Muktasari: Ajali zinazohusisha mabasi na malori zimeibua maswali kuhusu muda wa mapumziko ya madereva, hali ya magari, usalama wa mizigo, ubora wa miundombinu na utekelezaji wa sheria, huku wadau wakitaka mfumo mzima wa usafiri uchunguzwe. Dar es Salaam. Wimbi la ajali zinazohusisha mabasi na malori limeibua wasiwasi kuhusu usalama wa usafiri nchini, huku wadau wakisema kuwa chanzo cha matukio hayo hakiwezi kuhusishwa na uzembe wa madereva pekee.
Nchi 35 Afrika zakutana Dar kujadili mustakabali wa Saccos
Mtendaji Mkuu wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Hassan Mnyone akizungumza na waandishi wa habari,kuhusu mkutano wa 26 wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Afrika,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Coop Bank, Godfrey Ng'urah.
Nchi 35 Afrika zakutaka Dar kujadili mustakabali wa Saccos
Mtendaji Mkuu wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT), Hassan Mnyone akizungumza na waandishi wa habari,kuhusu mkutano wa 26 wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo Afrika,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Coop Bank, Godfrey Ng'urah.
Wakandarasi wanawake walalamikia masharti ya zabuni, malipo
Baadhi ya wakandarasi wanawake walioshiriki katika mkutano wa Chama cha Wakandarasi Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee uliopo jijini Dar es Salaam Muktasari: Wakandarasi wanawake wamelalamikia kuchelewa kwa malipo ya Serikali, kutolipwa riba na masharti ya zabuni yanayowalazimu kuunda vikundi. Waziri Masanja Kadogosa amesema kampuni zinapaswa kushindana kwa kuzingatia uwezo, huku PPRA ikieleza utaratibu wa kufuatilia madai ya malipo. Dar es Salaam.
Moto wateketeza vyumba 19 Tandika
Mmiliki wa nyumba Said Mazoea, akiangalia nyumba yake iliyoteketea kwa ajali ya moto iliyopo mtaa wa Chacha, Tandika wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam Muktasari: Moto waunguza vyumba 19 kati ya 36 na duka la vinywaji lenye thamani ya Sh2 milioni, huku chanzo kikichunguzwa na matumizi ya eneo hilo yakizua mjadala. Dar es Salaam.
Aliyepotea na mtoto wa miezi 10 Dar apatikana
Kaimu Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika ofisi za Jeshi la Polisi za jiji hilo kuhusu hali ya usalama. Muktasari: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limempata Angela Abaye (19), mfanyakazi wa ndani aliyeripotiwa kutoweka akiwa na mtoto wa miezi 10, huku likisema uchunguzi wa mauaji ya mwanafunzi Diana Sajilo ukiendelea. Dar es Salaam.
Wanafunzi walivyobuni suluhu kero za wananchi, Costech yazitolea kauli
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Telnolojia (COSTECH) Dk Amos Nungu (katikati kulia) akipokea maelwkezo kutoka kwa wanafunzi kuhusu ubunifu waliofanya kwa wiki nane za mafunzo ya masomo kwa vitendo (Field) kutoka vyuo mbalimbali nchi. Muktasari: Wanafunzi 79 wamegeuza mafunzo ya vitendo kuwa fursa ya ubunifu baada ya kubuni suluhisho tano za changamoto za jamii, zikiwamo taa za vijijini, kadi ya kidijitali ya kliniki na mfumo wa kurahisisha manunuzi madukani. Dar es Salaam.
Field training becomes launchpad for student innovation
Dar es Salaam. Instead of spending their field training carrying out routine tasks assigned by employers, 79 university students have turned the experience into an innovation platform, developing five solutions aimed at addressing community challenges and creating business opportunities. The students took part in an eight-week Talent Pool programme designed to equip them with critical thinking skills, help them identify challenges and turn them into innovative and commercially viable solutions.
Walimu 700 kuwa wakufunzi wa Tehama
Waziri wa mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angelah Kairuki akizungumza katika mafunzo ya Tehama kwa walimu wa sekondari wa umma yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kukutanisha walimu 700 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar Muktasari: Serikali imewataka walimu 700 waliopatiwa mafunzo ya Tehama kuwa wakufunzi wa wenzao, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza ujuzi wa kidijitali kwa watumishi wa umma na wananchi. Dar es Salaam.
Tanzania yahitaji Sh26 trilioni kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Waziri wa Fedha,Balozi Khamis Mussa Omar, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano Kuhusu Upatikanaji wa Fedha za Ufadhili wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi wa Mwaka 2026 (Tanzania Climate Finance Roundtable) chini ya kaulimbiu “Unlocking Climate Finance in the United Republic of Tanzania”, uliowakutanisha viongozi wa Serikali, washirika wa maendeleo, taasisi za fedha na sekta binafsi, uliofanyika Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Sekondari za jioni zilipokusanya kina baba na kinamama
Muktasari: Madarasa haya yaliwalenga vijana, watu wazima na makundi yaliyokuwa yamekosa fursa za elimu rasmi. Masomo yalifanyika jioni kwa sababu wanafunzi wengi walikuwa na kazi au majukumu mengine wakati wa mchana. Dar es Salaam. Alasiri ilipofika, shule za msingi hazikuwa zikifunga milango kabisa. Badala yake, baada ya wanafunzi wadogo kurudi nyumbani, madarasa yalijazwa na sura nyingine ya vijana na watu wazima waliokuja kutafuta elimu ya sekondari.
Wanafunzi Kinondoni Muslim ni ubabe, vituko
Muktasari: Kinondoni Muslim ilikuwa shule ya dini maarufu zaidi katika Mkoa wa Dar es Salaam miaka ya 1980 na 1990. Dar es Salaam. Ushindani wa shule za sekondari jijini Dar es Salaam miaka ya 1990 haukuishia kwenye uwanja wa michezo. Wakati mwingine, ushindani huo uligeuka kuwa mvutano na hata vurugu kati ya wanafunzi. Miongoni mwa matukio yaliyobaki kwenye kumbukumbu za wanafunzi wa wakati huo, ni mvutano uliowahi kutokea kati ya wanafunzi wa Kinondoni Muslim na Tambaza baada ya mchezo.
Mafunzo, ukaguzi suluhisho la usalama vituo vya mafuta – 3
Muktasari: Serikali imekuwa ikitumia Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kutoa elimu na huduma kwa makundi mbalimbali ya wafanyakazi. Dar es Salaam. Kuongezeka kwa vituo vya mafuta nchini kunahitaji kwenda sambamba na mfumo madhubuti wa usalama unaolenga kumlinda mfanyakazi tangu siku ya kwanza kazini, badala ya kusubiri ajali, ugonjwa au ukaguzi kubaini kasoro, imeelezwa.
Training, inspections crucial for improved safety at fuel stations
Dar es Salaam. The growing number of petrol stations in Tanzania needs to be matched by stronger safety systems that protect workers from their first day on the job, rather than waiting for accidents, illness or inspections to expose shortcomings. A Mwananchi investigation in Mbeya and Tanga regions found some filling station attendants working without safety shoes, gloves or masks, while others started work without training in fire safety, the use of fire extinguishers and emergency response.
DCEA yaonya magari ya maiti kutumika kusafirisha dawa za kulevya
Muktasari: DCEA imesema imebaini baadhi ya magari yanayosafirisha maiti kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kaskazini hutumika kusafirisha dawa za kulevya, ikiwamo mirungi na skanka, na imeonya itayakagua kila ipatapo taarifa za kiintelijensia. Dar es Salaam. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema baadhi ya magari yanayosafirisha maiti kwenda mikoa mbalimbali nchini yameanza kutumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kusafirisha mirungi, bangi na skanka.
Fuel station inspection lapses raise accountability questions
Dar es Salaam. Flip-flops, inadequate protective equipment and limited safety training among some fuel station workers are not simply individual shortcomings but signs of gaps in a system meant to protect people working in hazardous environments. In an industry where fuel and its vapour can ignite within seconds, worker safety depends on responsibilities that extend from employers to government institutions overseeing occupational health, safety and the operation of fuel stations.
Mapengo ukaguzi vituo vya mafuta yaibua uwajibikaji -2
Muktasari: Mfanyakazi ana wajibu wa kutumia vifaa anavyopewa, kufuata taratibu za usalama na kuripoti hatari anazoziona, lakini hilo haliwezi kumwondolea mwajiri jukumu la kuhakikisha vifaa na mafunzo vinapatikana. Dar es Salaam. Kandambili, ukosefu wa vifaa kinga na mafunzo ya usalama kwa baadhi ya wahudumu wa vituo vya mafuta nchini si changamoto ya mfanyakazi mmojammoja, bali ni dalili ya mapengo katika mfumo unaopaswa kuhakikisha kila anayefanya kazi katika mazingira hayo analindwa.
Concern as safety gaps leave fuel station workers exposed
Dar es Salaam. Some fuel station workers in Tanzania are working without protective footwear, gloves or masks and with little or no training on how to respond to fires, raising concerns over workplace safety in an industry that handles highly flammable substances.
Wahudumu vituo vya mafuta katikati ya tanuri la moto - 1
Prime Muhudumu wa kituo cha mafuta kilichopo Kiwira, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya akiwa amevaa sketi ambayo haijaorodheshwa katika mavazi ya kuvaa sehemu za kazi yenye mazingira hatarishi akiwa anamuhudumia mteja wa mafuta aliyefika kituoni hapo. Muktasari: Ukosefu wa ukaguzi wa mara kwa mara kwenye vituo vya mafuta umechangia kulegalega kwa utekelezaji wa sheria. Dar es Salaam.
Serikali yafanyia kazi changamoto Stendi ya Magufuli
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini(Latra), Dk Habibu Suluo akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliw ana Ofisi ya Msajili wa Hazini uliofanyika jijini Dar es Salaam. Muktasari: Latra imesema Serikali inaendelea kushughulikia changamoto za abiria na wasafirishaji baada ya mabasi ya mikoani kuhamishiwa Stendi ya Magufuli, huku ikiwataka wadau kutoa maoni na kusisitiza mawakala hawaruhusiwi kukamata vyombo vya usafiri. Dar es Salaam.
Latra yapiga marufuku mawakala kuwakamata bodaboda, bajaji
Muktasari: Yaonya mawakala kuchomoa funguo, kuwakamata bajaji na pikipiki; yasema jukumu lao ni kutoa leseni. Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) imewapiga marufuku mawakala wake kuwakamata madereva wa bajaji na pikipiki, kuwachomolea funguo au kufanya shughuli za utekelezaji wa sheria.
Watatu wauawa, 25 wakamatwa kwa vurugu za wakulima, wafugaji Tunduru
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya Muktasari: Matukio hayo yamesababisha uvamizi wa vijiji, kuchomwa kwa ofisi za Serikali, uharibifu na uporaji wa mali. Polisi imesema operesheni na upelelezi wa kuwakamata wengine bado unaendelea. Dar es Salaam. Watu watatu wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mfululizo wa matukio ya vurugu kati ya wakulima na wafugaji wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, yaliyosababisha pia kuchomwa kwa ofisi za Serikali na kuharibiwa kwa mali.
Show More
loading
Actions
Is this you?
As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.Get in touch with Devotha
Contact Devotha, search articles and posts on X, monitor coverage, and track replies from one place.
Learn more about Muck Rack