Is this you? As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.
Claim your profile
Articles by Fortune Francis
Uchaguzi ADC: Doyo akata rufaa kupinga kushindwa, Hamad Rashid afunguka
Muktasari: Doyo akata rufaa kupinga uchaguzi wa ADC, aeleza sababu akidai ni kukiukwa kwa katiba na kanuni za chama, aituhumu kamati ya uchaguzi pamoja na mwenyekiti aliyemaliza muda wake. Dar es Salaam. Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo amekata rufaa katika kamati ya rufaa ya chama hicho, kupinga uchaguzi uliofanyika, akidai kutoridhika na matokeo.
Msajili akana kuutambua uchaguzi wa TLP
Muktasari: Wakati ADC ikipata viongozi wapya, TLP imeitisha mkutano wa kumchagua mrithi wa Mrema, lakini Ofisi ya Msajili imekana kuutambua. Dar es Salaam. Wakati Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kikipata viongozi wapya, Chama cha Labour Party (TLP) kimefanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, huku Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ikisema haiutambua uchaguzi huo.
Itutu amdondosha Doyo uenyekiti ADC
Muktasari: Kati ya jumla ya kura zilizopigwa 192 Itutu amepata kura 121 dhidi ya Doyo aliyepata 70, huku moja ikiharibika. Dar es Salaam. Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), kimepata viongozi wapya wa kitaifa, huku aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Shabani Itutu akiibuka na ushindi kwa nafasi ya Mwenyekiti Taifa. Itutu amemshinda Doyo Hassan aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho. Uchaguzi huo wa nne wa ADC umefanyika leo Jumamosi Juni 29, 2024 katika ukumbi wa Lamada jijini Dar es Salaam.
ADC kupata viongozi wapya leo
Muktasari: Uchaguzi huo unalenga kuwapata viongozi wapya watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba yao, huku wagombea wawili wakitarajia kuchuana katika kinyang'anyiro hicho. Dar es Salaam. Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed akimekipongeza Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), kwa kuweka utaratibu wa ukomo wa uongozi licha ya uchanga wake.
Jeshi la Polisi lapiga marufuku kumiliki gobore, laruhusu Shortgun
Muktasari: Jeshi la Polisi nchini limetahadharisha mambo matano kuhusiana na umiliki wa silaha, kampuni binafsi za ulinzi, wanaomiliki silaha za mirathi pamoja na silaha zaisizolipiwa leseni wapewa muda kujisalimisha. Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limepiga marufuku kampuni binafsi za ulinzi zinazotumia silaha zilizotengenezwa kienyeji (Gobore), badala yake imeshauriwa kufuata utaratibu wa kisheria wa kumiliki silaha aina ya “shotgun” kwani ndizo zinazoruhusiwa kutumika kwa shughuli za ulinzi.
Mbowe: CCM wanajua uchaguzi huru, haki hawatoboi
Muktasari: Chadema yaendelea na Operesheni +255 Mkoa wa Manyara ikiwa ni siku ya saba tangu kuanza kwa operesheni hiyo itakayotumia siku zaidi ya 20 kwenye mikoa minn ya Kanda ya Kaskazini. Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejiahakikishia ushindi katika chaguzi zijazo huku kikibainisha kuwa uchaguzi huru Chama cha Mapinduzi (CCM) hawatatoboa.
Majaliwa aeleza alivyofanya kazi na Nzunda
Muktasari: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aongoza waombolezaji kuaga mwili wa Tixon Nzunda, jijini Dar es Salaam. Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Juni 18, 2024.
Masoud Kipanya kumdai Mwijaku fidia ya Sh5 bilioni
Muktasari: Wakili wa Masoud adai mteja wake amekashifiwa, kushushiwa heshima Dar es Salaam. Siku chache baada ya kusambaa taarifa zinazomuhusu Ali Masoud 'Masoud Kipanya' kwenye mitandao ya kijamii, Wakili Mwandamizi Alloyce Komba amesema wanakusudia kwenda mahakamani kudai fidia ya Sh5 bilioni. Taarifa inayodaiwa kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii na Burton Mwemba maarufu 'Mwijaku' inaelezwa kuwa imemkashfu na kumshushia heshima Masoud.
LHRC yaanika mafanikio yake kwa mwaka 2023
Muktasari: LHRC yasema asilimia 90 ya mapendekezo iliyoyatoa yalijumuishwa kwenye ripoti ya Tume ya Haki Jinai. Dar es Salaam. Miezi 11 tangu Tume ya Haki Jinai ilipowasilisha taarifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema asilimia 90 ya mapendekezo waliyoyatoa yalijumuishwa kwenye ripoti.
Makundi maalumu yapewa neno INEC ikijiandaa kwa uchaguzi
Muktasari: Wenye ulemavu, wajawazito na wenye watoto wachanga waandaliwa utaratibu maalumu Dar es Salaam. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeyataka makundi maalamu, wakiwamo watu wenye ulemavu kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura, kutokana na mifumo kuboreshwa. Tume imesema wapigakura wengi wamekuwa hawajiandikishi, wakiwamo wenye ulemavu, wajawazito na wenye watoto wachanga.
CUF yajipanga kudai Katiba mpya, Tume Huru ya Uchaguzi
Dar es Salaam. Chama cha Wananchi (CUF) kimesema wakati Taifa likielekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kinatarajia kufanya mazungumzo na vyama vingine vya siasa kuhusu suala la Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Uamuzi huo wa CUF umechochewa na madai kwamba miswada iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais kuwa sheria, ni danganya toto kwa kuwa maoni ya wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa siasa yalipuuzwa.
Wadau wataka sheria mpya leseni za usafirishaji
Muktasari: Kwa kuwa sekta ya usafirishaji ina umuhimu katika uchumi, wadau wanaamini sheria mpya ya utoaji leseni haitarahisisha tu shughuli, pia itaimarisha usalama, ushindani na ubora wa huduma Dar es Salaam. Wadau wa usafirishaji wametoa wito kwa Serikali kutunga sheria mpya ya leseni za usafirishaji ili kutengeneza mazingira bora ya utendaji katika sekta hiyo.
Doyo atangaza kumrithi Hamad Rashid ADC
Muktasari: Kwa mujibu wa Katiba ya ADC kiongozi huongoza kwa vipindi viwili vya miaka mitano baada ya kumaliza hataruhusiwa kugombea. Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Doyo Hassan Doyo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya uwenyekiti wa chama hicho, kinachoongozwa na Hamad Rashid. Kwa mujibu wa katiba ya chama hicho nafasi ya kiongozi ni kuongoza vipindi viwili vya miaka mitano.
Mahujaji 3,300 wanaoenda kuhiji wapewa somo
Muktasari: Sheikh Hamid Jongo amewataka wote watakaoenda hijja kuziacha familia zao vizuri kisaikolojia na kuwatoa wasiwasi. Dar es Salaam. Mahujaji wanaokwenda kuhiji Makka wametakiwa kuwa makini na kufuata maelekezo ya viongozi ili kunufaika na nguzo hiyo muhimu kati ya tano za kiislamu. Pia, wametakiwa watakapokuwa hijja kujikita katika ibada kwa ajili ya mwenyezi Mungu.
Lissu ‘atia mguu’ jimbo la Mwigulu
Muktasari: Aanza ziara yake jimboni akihimiza wananchi kujipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na uichaguzi mkuu mwakani. Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu ameanza ziara ya wiki tatu Mkoa wa Singida ambako atafanya mikutano ya hadhara katika kata zote kwenye kila wilaya.
Wahitimu watakiwa kutumia taaluma zao kujiajiri
Muktasari: Wahitimu wa kozi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wametakiwa kutumia taaluma walizopata kujiajiri, badala ya kusubiri tu ajira rasmi serikalini na sekta binafsi. Dar es Salaam. Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wametakiwa kutosubiri kuajiriwa serikalini au katika sekta binafsi, bali watafute namna ya kutumia ujuzi walioupata katika masomo yao kujipatia kipato.
Necta yafuta maswali ya kuchagua hisabati mitihani shule za msingi
Muktasari: Masomo mengine yanayotarajiwa kuachana na mfumo huo kwa ngazi ya sekondari ni biolojia, fizikia na Kiingereza. Serikali inazidi kufanyia kazi maoni ya wadau wa elimu kwa lengo la kuboresha mfumo wa elimu nchini. Sasa imetangaza kuachana na mfumo wa kutahini somo la hisabati katika mtihani wa kumaliza darasa la saba, kwa kutumia utaratibu wa maswali ya kuchagua.
Mwenge wa Uhuru wamulika ununuzi wa umma
Muktasari: Kiongozi mbio za Mwenge wa Uhuru asisitiza zabuni za ununuzi kutangazwa kwenye mfumo wa kidijitali Dar es Salaam. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024, Godfrey Mnzava ameshauri zabuni za ununuzi wa umma kutangazwa kwenye mfumo ili kupunguza malalamiko na manung'uniko.
Mitihani ya kidato cha sita kuanza kesho
Muktasari: Watahiniwa 113,504 wa kidato cha sita na ualimu ngazi ya cheti na stashahada wanatarajiwa kuanza mitihani yao kesho Mei 6 mwaka 2024. Dar es Salaam. Jumla ya watahiniwa 113,504 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha sita, kuanzia kesho Mei 6 mwaka huu huku ikitarajiwa kumalizika Mei 24. Mtihani huo wa kidato cha sita, utafanyika kwenye jumla ya shule 931 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 258.
Ujenzi holela unavyokwamisha uokoaji raia wakati wa majanga
Muktasari: Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa miaka miwili mfululizo 2020/21 na 2022/23 zimebainisha kasoro na changamoto zinazolikabili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ikiwemo vifaa Dar es Salaam. Miongoni mwa sababu za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kushindwa kufika eneo la tukio ni pamoja na mipango miji, huku sababu nyingine ikielezwa ni miundombinu kutokuwa rafiki.
Watu watano mbaroni wakidaiwa kuiba runinga 35
Muktasari: Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuendelea kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa wahalifu, wanaojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria Dar es Salaaam. Wakati matukio ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali vya ndani yakiripotiwa, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia Esahu Francis (27) mkazi wa Makumbusho na wenzake wanne kwa kukutwa na runinga 35 za wizi.
Kimbunga Hidaya: Usafiri majini na angani waendelea kama kawaida
Muktasari: Licha ya tahadhari kutolewa shughuli katika bandari ya Dar es Salaam na sekta za anga ikiwemo safari zinaendelea kama kawaida. Dar es Salaam. Licha ya tahadhari kutolewa kwa baadhi ya mikoa nchini Tanzania kuhusu kimbunga ‘Hidaya‘ shughuli katika bandari ya Dar es Salaam zimeendelea kama kawaida ikiwemo huduma za usafiri wa majini. Mbali na usafiri wa majini wa anga pia umeendelea kama kawaida.
CMA, TIC waingia makubaliano kupunguza migogoro ya wawekezaji, wafanyakazi
Muktasari: Katika makubaliano hayo yatahakikisha uchumi unakua kwa kutatua migogoro ya wawekezaji wanapokuja kuwekeza nchini Tanzania. Dar es Salaam. Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wameingia makubaliano ya ushirikiano katika kupunguza migogoro ili kuboresha mazingira kwa wawekezaji nchini Tanzania.
Moto wateketeza nyumba Tabata, gari la Zimamoto lakwama kuifikia
Muktasari: Wapangaji washindwa kuokoa chochote, msongamano unaotokana na ujenzi holela wa makazi wakwamisha gari la Zimamoto kufika eneo la tukio. Dar es Salaam. Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika umeteketeza nyumba eneo la Tabata Kisiwani, Dar es Salaam. Moto huo uliozuka leo Alhamisi Mei 2, 2024 saa moja usiku umeteketeza nyumba na mali zote zilizokuwamo ndani.
Kisebengo kizimbani akidaiwa kusafirisha heroini na kokeni
Dar es Salaam.  Mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, Nasibu Kisebengo (44), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini na kokeni kinyume na sheria. Kisebengo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumanne Aprili 30, 2024 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Happy Mwakanyamale mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swalloh.
Familia ya Zuchy yaeleza ndoto aliyokuwa nayo ndugu yao, ratiba ya mazishi
Muktasari: Mwili wa Noel Mwingira, maarufu Zuchy unatarajiwa kuzikwa Jumatatu, Aprili 29, katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kaka yake ameelezea ndoto aliyokuwa nayo siku za usoni. Dar es Salaam. Wakati Jeshi la Polisi nchini Tanzania likiwataka watu wenye taarifa tofauti juu ya kifo cha Noel Mwingira, maarufu Zuchy wazipeleke zifanyiwe kazi, John Msabaha, mdogo wa marehemu amesema ndugu yake amefariki dunia akiwa mbioni kufungua kampuni inayojishughulisha na masUala ya vipodozi.
Polisi yaita wenye taarifa kuhusu kifo cha Zuchy
Muktasari: Jeshi la Polisi limetaka mwenye taarifa tofauti zinazohusu tukio la ajali ya bodaboda iliyotokea na kusababisha kifo cha Noel Mwingira, maarufu Zuchy azipeleke ili hatua zichukuliwe. Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini Tanzania limewataka watu wenye taarifa tofauti juu ya ajali ya bodaboda iliyotokea alfajiri ya jana Ijumaa Aprili 26, 2024, eneo la Makonde, mkoani Dar es Salaam na kusababisha kifo cha Noel Mwingira, maarufu Zuchy wazipeleke zifanyiwe kazi.
Mbowe asisitiza muungano wa Serikali tatu
Muktasari: Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesisitiza msimamo wa chama hicho ni kuwa na muungano wa Serikali tatu, ikiwamo Serikali ya Tanganyika. Musoma/Dar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema licha ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar kutimiza miaka 60, bado unahitaji maboresho, akipendekeza muundo wa Serikali tatu ikiwamo ya Tanganyika.
‘Uhusiano na mawasiliano kada muhimu za maendeleo’
Muktasari: Rais wa PRST, Asah Mwambene amesema tayari mchakato kwa ajili ya kuanzisha, sheria ya kusimamia taaluma ya maofisa habari serikalini umeanza Dar es Salaam. Kada ya maofisa uhusiano na mawasiliano, imetajwa kuwa muhimu kutokana na mchango wake katika ukuzaji wa uchumi.
TMA yatoa angalizo la mvua mikoa mitano
Muktasari: Wakati mvua ikiwapa biashara wachuuzi kwenye vijiwe vya kahawa, abiria walalama adha ya usafiri. Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya hali mbaya ya hewa inayoweza kujitokeza kwa siku tano na kuathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi. Taarifa iliyotolewa na TMA leo Alhamisi Aprili 4, 2024 imetoa angalizo hilo kwa maeneo machache ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia; Lindi, Mtwara na visiwa vya Unguja na Pemba.
VIDEO: Adha ya daraja inavyowatesa wakazi Pwani, Dar
Muktasari: Daraja hilo ambalo ni kiunganishi cha pande mbili kinategemewa hasa na wananchi wa kata ya Pangani ambao hununua mahitaji yao upande wa Kibwegere jijini Dar es Salaam. Pwani. Wananchi wa kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani na Kibwegere Wilayani Ubungo, Dar es Salaam, wameiomba Serikali kuwatengenezea daraja, ili kuondokana na adha wanayoipata kipindi cha mvua na kusababisha kukatika kwa mawasiliano.
Adha ya daraja inavyowatesa wakazi Pwani, Dar
Muktasari: Daraja hilo ambalo ni kiunganishi cha pande mbili kinategemewa hasa na wananchi wa kata ya Pangani ambao hununua mahitaji yao upande wa Kibwegere jijini Dar es Salaam. Pwani. Wananchi wa kata ya Pangani Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani na Kibwegere Wilayani Ubungo, Dar es Salaam, wameiomba Serikali kuwatengenezea daraja, ili kuondokana na adha wanayoipata kipindi cha mvua na kusababisha kukatika kwa mawasiliano.
Polisi: Tutaowakamata kesho wenye namba 3D, kuwafikisha mahakamani
Muktasari: Operesheni dhidi ya matumizi ya namba za 3D kwenye magari imeanza nchi nzima, na hatua inayofuata ni kukamatwa, kuwekw mahabusu na kufikishwa mahakamani. Dar es Salaam. Baada ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kuanza operesheni kwa watu walioweka namba zilizoongezwa ukubwa ‘3D’ kwa kuwatoza faini, hatua itakayofuata kuanzia kesho Jumamosi, Machi 16, 2024 ni kuwakamata, kuwaweka mahabusu na kuwafikisha mahakamani.
Polisi waanza msako kung’oa namba za 3D kwenye magari
Muktasari: Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, limeanza kuwachukulia hatua watu waliokaidi kuondoa vibao vya namba za usajili wa magari aina ya 3D kwa hiari baada ya muda uliokuwa umetolewa kumalizika. Dar es Salaam. Baada ya wamiliki wa magari kupewa wiki mbili ya kuondoa kwa hiari namba za uzajili wa magari zilizoongezwa ukubwa maarufu kwa jina la 3D, Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani, limeanza kuwachulia hatua waliokaidi agizo hilo.
Mufti ataja mchango wa Mzee Mwinyi Bakwata
Muktasari: Dua hiyo imefanyika katika Msikiti wa Mohamed wa sita Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahaman Kinana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu. Dar es Salaam. Baraza la Waislamu Tanzania Bakwata limefanya dua maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya pili, hayati Ali Hassan Mwinyi, huku likieleza mchango alioutoa kwa taasisi hiyo.
Bakwata kumwandalia dua maalumu Mzee Mwinyi
Muktasari: Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, ameelezea nia ya dua hiyo na kumuenzi Mwinyi kwa mchango wake kwa Waislamu na taifa kwa ujumla. Dar es Salaam. Wakati Taifa leo likihitimisha siku ya saba za maombolezo ya kifo ch Rais mstaafu, hayati Ali Hassan Mwinyi, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limetangaza kuandaa dua maalumu ya kumuombea kiongozi huyo.
Wajitokeza kuzitambua pikipiki zao zilizokamatwa na polisi
Muktasari: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu watatu wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa pikipiki, huku wamiliki walijitokeza kuzitambua na kusimulia zilivyoibwa Dar es Salaam. Wakati Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likiwashikilia watu wawili wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa wizi wa pikipiki, baadhi ya wamiliki wamejitokeza kuzitambua na kueleza namna zilivyoibiwa.
Yaliyojificha nyuma ya watoto wauza mifuko Kariakoo
Dar es Salaam. Majira ya mchana, saa sita yenye jua kali ndani ya soko la Kariakoo, nikifanya habari ya maandalizi ya msimu mpya wa masomo, wakati nikiendelea na mahojiano na mmoja wa wauzaji, navutiwa na viatu alivyokuwa akiuza. Baada ya mazungumzo kumalizika, naamua kununua lakini nafsi yangu inaniambia nahitaji mfuko mzuri kwa ajili ya kuvibeba ili mtu asijue kilichomo ndani yake ndipo muuzaji anagundua hilo.
Kitambaa Cheupe ya Tabata yateketea, mashuhuda wasimulia
Muktasari: Mkurugenzi wa Baa ya Kitambaa Cheupe Jesca Kikumbi amesema anachomshukuru Mungu baada ya tukio la moto kutokea hakuna yeyote aliyeumia Dar es Salaam. Baa maarufu ya Kitambaa Cheupe iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam imeteketea kwa moto chanzo kikidaiwa ni fundi wa kuchomolea. Kwa mujibu wa Jacksoni Mkami, fundi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) walipofika eneo la tukio walichunguza kilichosababisha tukio la moto nakubaini kuna mafundi waliokuwa wanafanya kazi yakuchomea.
Polisi wapewa angalizo usimamizi wa mifumo
Muktasari: Mambosasa asema cheo si mapambo wala zawadi, ni stahili ya mtumishi anayetimiza wajibu wake. Dar es Salaam. Askari wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini (DPA), wametakiwa kusimamia mifumo ya jeshi hilo na kuangalia changamoto zilizoainishwa kwenye ripoti ya Tume ya Kuboresha Mifumo na Taasisi za Haki Jinai nchini. Pia, wametakiwa kuwekeza katika majukumu yanayotimiza dhima nzima ya jeshi hilo, ili wote wanufaike na matunda ya kazi wanayoifanya.
UN Global Compact Network, wadau wajadili kufikia malengo endelevu
Muktasari: Malengo hayo yanaangalia ni njia gani nyepesi na ya haraka kufikia suala zima la usawa wa kijinsia, mabadiliko ya tabianchi, ufadhili na uwekezaji Dar es Salaam. Ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030, Shirika la UN Global Compact Network chapa ya Tanzania limekutana na wadau kuangalia njia nyepesi ya kufikia malengo hayo.
Wengi wajitokeza kuaga mwili wa Ole Mushi
Muktasari: Dada wake aishukuru Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kwa misaada yao. Dar es Salaam. Mwili wa mchambuzi na mchangiaji mada kwenye mijadala mitandaoni, Thadei Ole Mushi umeagwa jijini Dar es Salaam, huku familia ikiishukuru Serikali na wadau kwa namna walivyojitoa kumsaidia ndugu yao.
Latra yajipanga nauli treni za SGR Dar - Dom
Muktasari: Mamlaka ya Usafiri Ardhini (Latra) inakamilisha, upangaji wa viwango vya nauli za treni za mwendo wa haraka, vitakavyotumika baada ya huduma kuanza rasmi kati ya Dar es Salaam na Dodoma. Dar es Salaam. Mamlaka ya Usafiri Ardhini (Latra) inakamilisha, upangaji wa viwango vya nauli ya treni za mwendo wa haraka vitakavyotumika baada ya huduma kuanza rasmi kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Wawili mbaroni kwa tuhuma za utekaji, mauaji Dar
Muktasari: Tukio hilo limetokea wakati kukiwa na taarifa za watu kutoweka na kutekwa maeneo mbalimbali nchini. Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya Mohamed Ameir (35), mkazi wa Magomeni- Mwembechai wilayani Kinondoni. Taarifa iliyotolewa jana Februari 2, 2024 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro inaeleza mwili wa Ameir umekutwa katika fukwe za Kigamboni, Februari mosi, 2024.
Madiwani, Mwenyekiti CCM watofautiana mifugo inayozurura, uchaguzi ukihusishwa
Muktasari: Mwenyekiti CCM apingana na uamuzi wa Baraza la Madiwani, ataka wenye mifugo inayozagaa kutokamatwa kwa sababu wanaelekea kwenye uchaguzi, na wamiliki wa mifugo hiyo ndiyo wapigakura wao. Dar es Salaam. Wakati joto la uchaguzi likiendelea kupanda, Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kigamboni, Sikunjema Shaban ametofautiana na uamuzi wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichokubaliana kwamba mifugo inayozagaa hovyo ikamatwe.
Chalamila apongeza Polisi kufanikisha maandamano Chadema
Muktasari: Januari 24, 2024 Chadema iliweka rekodi kwa kufanya maandamano ya amani yakilenga kufikisha ujumbe kwa Umoja wa Mataifa. Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikisha maandamano ya Chadema jijini hapa. Jana, Januari 24, 2024, Chadema iliweka rekodi kwa kufanya maandamano ya Amani Jijini Dar es Salaam yakiongozwa na viongozi wakuu wa chama hicho.
Halmashauri ya Temeke yatishia kufungia stendi binafsi
Muktasari: Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabely amesema wameshatoa notisi kwa wamiliki wa stendi hizo kuhakikisha wanazifanyia usafi na kuziboresha kabla hawajazifunga Dar es Salaam. Wakati Mkoa wa Dar es Salaam ukitangaza maeneo hatarishi yanayoweza kukumbwa na Ugonjwa wa Kipindupindu, Halmashauri ya Wilaya ya Temeke imetishia kuzifungia stendi zinazomilikiwa na watu binafsi watakaoshindwa kuzifanyia ukarabati.
Mabasi Kilimanjaro ruksa kuendelea na safari
Muktasari: Januari 6 mwaka huu, Latra ilisitisha leseni na ratiba za mabasi 35 ya kampuni ya Kilimanjaro Truck Limited baada ya kubainika kukiuka masharti ya leseni. Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imeruhusu leseni na ratiba za mabasi 35 ya kampuni ya Kilimanjaro Truck Limited kuendelea kutumika baada ya kutimiza masharti.
ACT- Wazalendo yasisitiza miswada izingatie maoni ya wadau
Muktasari: ACT-Wazalendo imewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Tanga, chama hicho kitaendelea kusukuma uboreshaji wa miswada hiyo ili nchi iweze kuwa na uhuru wa kisiasa kama Taifa Dar es Salaam. ACT- Wazalendo imeendelea kuisisitiza Serikali kuhakikisha miswada mitatu ya sheria za uchaguzi iliyopelekwa bungeni kuboreshwa inaakisi maoni na mapendekezo ya wadau wa demokrasia nchini.
ACT- Wazalendo yasisitiza miswada ya izingatie maoni ya wadau
Muktasari: ACT-Wazalendo imewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Tanga, chama hicho kitaendelea kusukuma uboreshaji wa miswada hiyo ili nchi iweze kuwa na uhuru wa kisiasa kama Taifa Dar es Salaam. ACT- Wazalendo imeendelea kuisisitiza Serikali kuhakikisha miswada mitatu ya sheria za uchaguzi iliyopelekwa bungeni kuboreshwa inaakisi maoni na mapendekezo ya wadau wa demokrasia nchini.
Show More
loading
Actions
Is this you?
As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.Get in touch with Fortune
Contact Fortune, search articles and posts on X, monitor coverage, and track replies from one place.
Learn more about Muck Rack