Is this you? As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.
Claim your profile
Articles by Sharon Sauwa
Rais Samia kufungua kongamano la elimu bila kikomo
Muktasari: Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) inatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ambapo itawakutanisha wadau wa elimu ndani na nje kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na elimu bila ukomo. Dodoma. Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) itawakutanisha wadau wa elimu katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, huku miongoni mwa malengo yakielezwa ni kuangazia umuhimu wa kujua kusoma na kuandika katika kujifunza bila ukomo.
INEC, wanasiasa wafundana
Muktasari: Wakati kipenga cha uchaguzi mkuu kimeshapulizwa, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na vyama vya siasa wazungumza Dodoma. Wakati Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiwataka wanasiasa na wafuasi wao kufanya kampeni za kistaarabu, baadhi ya vyama vya siasa vimetaka ofisi za tume hiyo kuwa wazi kabla na baada ya uchukuaji na urejeshaji fomu za kuomba uteuzi.
Samia alivyoongoza kumbukumbu ya mashujaa
Muktasari: Brigedia Jenerali Francis Mndolwa awataka waandishi wa habari nchini Tanzania kuwa wazalendo ili amani iliyopo iendelee kudumu. Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amewaongoza Watanzania kuadhimisha Siku ya Mashujaa. Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali Mtumba, mkoani Dodoma yalikofanyika maadhimisho hayo leo Julai 25, 2025 Rais Samia amepokewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda.
Samia mgeni rasmi maadhimisho ya mashujaa
Muktasari: Madhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa yatafanyika kesho Julai 25, 2025 katika Viwanja vya kumbukumbu ya mashujaa vilivyopo Mtumba jijini Dodoma, huku Serikali ikitoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi. Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa itakayofanyika kesho Julai 25,2025 Mtumba, jijini Dodoma.
Aliyeuawa kwa risasi na polisi azikwa
Muktasari: Frank Sanga aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi waliokuwa doria amezikwa huku wachungaji, viongozi wakitoa kauli. Dodoma. Mwili wa Frank Sanga (34) aliyefariki dunia kwa kupigwa na risasi umezikwa leo huku wachungaji wa Kanisa la Anglikana wakitaka Serikali isimamie mambo hayo yasijirudie kwa sababu yanaiumiza jamii. Mbali na vilio vilivyotanda nyumbani hadi kanisani, baadhi ya ndugu walipoteza fahamu baada ya kuona mwili wa ndugu yao.
Tanzania explains suspension of nine UDOM education programmes
Dodoma. The government has clarified that the suspension of nine undergraduate teacher education programmes at the University of Dodoma (UDOM) aims to improve the competence of future teachers by restructuring course content to focus more on subject mastery. This follows UDOM’s recent announcement that it will not admit students into the affected programmes for the 2025/26 academic year.
Serikali yatoa sababu kusitishwa kozi tisa UDOM
Muktasari: Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ametoa ufafanuzi kuhusu kusitishwa kwa kozi UDOM, huku akieleza takribani wanafunzi 1,000 walikuwa wameshaomba kudahiliwa katika kozi hizo. Dodoma. Siku chache baada ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kutangaza kusitisha udahili kwa kozi tisa za shahada ya kwanza kwenye elimu ya ualimu kwa mwaka 2025/26, Serikali imesema lengo ni kuongeza umahiri wa walimu wanaozalishwa kwenye chuo hicho.
Canada wamwaga mabilioni miradi ya elimu
Muktasari: Miradi mitatu kuwanufaisha vijana katika kuboresha maisha yao kiuchumi na lishe shuleni kwa mikoa ya Lindi na Mtwara. Dodoma. Serikali ya Canada imetangaza ufadhili kwenye miradi mitatu yenye thamani ya Sh90 bilioni (sawa na Dola za Marekani milioni 32), ikihusisha kuboresha lishe shuleni kwa wanafunzi 65,000 wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
University of Dodoma suspends admission into nine teacher education degree programmes
Dodoma. The University of Dodoma (Udom) has suspended admissions into nine undergraduate teacher education programmes for the 2025/2026 academic year, citing ongoing consultations with regulatory authorities.
Arusha Airport gets set for 24-hour flight operations
Dodoma. Arusha Airport, located in Kasongo, Arusha city, will begin 24-hour flight operations starting December 2025. Besides, Sh5.93 billion has been paid as compensation to 187 residents affected by the construction of Manyara Lake Airport. Iringa Regional Commissioner, Kenani Kihongosi, revealed this on Sunday, July 20, 2025, while highlighting the government’s achievements in his region.
UDOM yasitisha kozi tisa za elimu ya ualimu
Muktasari: Kwa mujibu wa tangazo la chuo hicho, chuo hakitodahili wanafunzi wanaoomba kozi hizo katika mwaka wa masomo wa 2025/26. Dodoma. Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kimesisitisha udahili wa programu tisa za shahada ya kwanza ya elimu ya ualimu katika mwaka wa masomo wa 2025/2026.
Uwanja wa ndege Arusha kutoa huduma saa 24
Muktasari: Serikali inafanya ukarabati na ujenzi wa viwanja viwili vya ndege jijini Arusha. Dodoma. Uwanja wa ndege wa jijini Arusha ulioko eneo la Kisongo, utaanza kutoa huduma za kuruka na kutua ndege saa 24, Desemba mwaka huu. Mbali na hilo, Sh5.93 bilioni zimetumika katika kuwalipa fidia wananchi 187 watakaopisha ujenzi wa Uwanja cha ndege Ziwa Manyara.
INEC yatoa vibali vya uangalizi na elimu ya mpigakura
Muktasari: Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani yanaendelea huku Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiweka wazi waliopewa vibali vya uangalizi na utoaji elimu ya uraia. Dodoma. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa vibali 164 kwa taasisi na asasi za kiraia kutoa elimu ya mpigakura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani 2025.
Siri nyuma ya mchujo wa CCM kusogezwa
Muktasari: Wachambuzi wa siasa nchini, wasema huenda ahirisho hilo linatokana na kauli na mnyukano wa ndani kwa ndani wa makada wa CCM unaofukuta pamoja na sababu zilizotolewa na CCM kuhusu idadi kubwa ya watiania waliojitokeza. Dodoma/Dar. Mambo ni mengi na muda ni mfupi kwenye ulingo wa siasa za Tanzania kwa sasa. Ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) presha kwa makada waliotia nia kuwania uteuzi wa kugombea uwakilishi na ubunge imeendelea kupanda na kushuka.
Sirro afunguka hali ya usalama Kigoma
Muktasari: Baada ya wahalifu kuyateka magari, kupora na kuwajeruhi abiria, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro ameelezea hali ilivyo mkoani huo. Dodoma. Siku chache baada ya tukio la utekaji wa magari na uporaji kutokea Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi linaendesha operesheni mkoa mzima kuwabaini wahusika kisha kuwafikisha mahakamani.
Kiwanda cha chaki Maswa chaanza majaribio ya uzalishaji
Muktasari: Katoni za chaki 11,884 zatengenezwa kama majaribio katika kiwanda cha kimkakati cha kutengeneza chaki na kuuzwa ndani na nje ya nchi. Dodoma. Kiwanda cha kimkakati cha kutengeneza chaki kimeanza majaribio ya uzalishaji ambapo katoni za chaki 11,884 zenye thamani ya Sh19.4 milioni zimezalishwa na kuuzwa ndani na nje ya nchi. Kiwanda hicho kimejengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kwa gharama ya Sh8.09 bilioni.
Hospitali iliyoanza kujengwa 1975, yaanza kutoa huduma
Muktasari: Katika kuimarisha huduma za afya nchini, Serikali imewezesha kuanza kazi kwa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mkoani Mara, iliyojengwa kwa zaidi ya miaka 45. Dodoma. Ujenzi wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ya Mkoa wa Mara iliyoanza kujengwa mwaka 1975, imeanza kutoa hudumu huku ujenzi wake ukiwa umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika miaka miwili ijayo.
Mbowe afunguka kuhusu Dira 2050
Muktasari: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua Dira 2050 huku Mwenyekiti wa zamani wa Chadema, Freeman Mbowe akiichambua kwa kifupi. Dodoma. Wadau wamepongeza hatua ya ushirikishaji wa rika zote katika maandalizi ya Dira 2050 huku Mwenyekiti wa zamani wa Chadema, Freeman Mbowe akieleza kusikitishwa na sehemu ya dira hiyo. Wadau wametoa maoni yao leo Alhamisi Julai 17, 2025 baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua dira hiyo itakayoanza kutekelezwa Julai Mosi, 2026.
Profesa Kitila alivyoichambua Dira 2050
Muktasari: Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji imetaja malengo mahususi, shabaha, misingi mikuu , vichocheo vitano vinavyoweza kurahisisha mageuzi ya uchumi katika Dira 2050. Dodoma. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema malengo mahususi ya Dira 2050 ni kuifanya Tanzania ifikie hadhi ya uchumi wa kipato cha ngazi ya juu.
Mikakati ya kuongeza kasi kupunguza vifo vya watoto wachanga yatajwa
Muktasari: Wadau wa masuala ya watoto wametaja mikakati inayohitajika kufanywa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano. Dodoma. Wadau wa masuala ya watoto wametaja mikakati itakayosaidia kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya watoto waliochini ya miaka mitano ikiwemo lishe, afya ya mama na mtoto kwa kuwajengea uwezo wahudumu wa afya.
Utiririshaji wa maji taka migodi midogo bado changamoto
Muktasari: Serikali imetaja mikakati ya kudhibiti utirishaji wa majitaka kutoka katika mabwawa ya maji na tope sumu ili kuepuka athari za kimazingira. Dodoma. Wizara ya Maji imesema bado migodi midogo inakabiliwa na changamoto ya utiririshaji wa maji taka na hivyo kusababisha athari kwenye vyanzo vya maji.
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 kuzinduliwa kesho kutwa
Muktasari: Dira hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Mipango iliundwa na Serikali kwa Sheria ya Tume ya Mipango ya Taifa mwaka 2023 na ina majukumu 20 ikiwamo usimamizi wa uchumi nchini na miongozo ya muda mrefu. Dodoma. Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk Fred Msemwa amesema mchakato wa kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 ulioanza Aprili, mwaka 2023 umekamilika na uzinduzi wake unatarajiwa kufanyika kesho kutwa.
Mabishano ya tozo yakwamisha Tanga kufikia malengo
Muktasari: Mkoa wa Tanga umefikia asilimia 95 ya makusanyo waliyopangiwa katika mwaka 2024/25 huku kiasi kilichobakia kikitarajiwa kufikiwa mara baada ya usuluhishi wa mambo ya tozo utakapokamilika. Dodoma. Mabishano ya tozo katika bidhaa zinazozalishwa na madini, yamesababisha Mkoa wa Tanga kushindwa kufikia lengo walilopangiwa katika makusanyo kwa mwaka 2024/25. Aidha, wastani wa pato la mtu mmoja mmoja kwa mwaka limeongezeka kutoka Sh2.7 milioni mwaka 2020 hadi Sh3.4 milioni kwa mwaka 2024.
Wanafunzi Udom wanavyolipiana ada
Muktasari: Ubunifu huo unahusisha mpango wa hatifungani ili kupata fedha za kuwalipia ada wanafunzi wanaokumbana na changamoto za kukosa ada. Dodoma. Licha ya jitihada za Serikali kuhakikisha wanafunzi wote waliodahiliwa kujiunga na elimu ya juu wanapata mikopo, bado wengine wameshindwa kunufaika na utaratibu huo na kukatisha ndoto zao.
Kampuni za kimataifa 15 kuwekeza kongani Buzwagi
Muktasari: Kongani maalumu la kimataifa la sekta ya madini la Buzwagi, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga limepata wawekezaji. Dodoma. Serikali imesema kampuni 15 za kimataifa zimeonyesha nia ya kuwekeza katika kongani maalumu la kimataifa la sekta ya madini, ambalo limeanzishwa kwenye eneo ulipokuwa Mgodi wa Buzwagi Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Wanachama CWT wataka kibali cha kuwashtaki viongozi
Muktasari: Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imetoa siku 14 kwa wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwamo viongozi kujibu hoja za wanachama wenzao Dodoma. Wanachama watatu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wamefungua shauri katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, wakiomba kibali cha kufungua shauri la jinai kwa walalamikiwa wanne wakiwamo viongozi chama hicho. Mbali na hilo, Mahakama hiyo imetoa siku 14 kwa walalamikiwa kujibu hoja kabla ya kutoa uamuzi wa kama shauri hilo lifunguliwe au la.
Local production of rapid test kits for HIV, syphilis and hepatitis on the cards
Dodoma. Tanzania is set to begin local production of medical rapid test kits for HIV, syphilis and hepatitis by August 2026, following a new agreement signed with global health technology firm ABBOTT. Speaking during the signing ceremony yesterday, Health minister Jenista Mhagama said the move aligns with the ministry’s 2025/26 budget priorities, particularly the promotion of local manufacturing of medicines and medical equipment.
CCM waanza mchakato uteuzi ngazi ya Taifa
Muktasari: Baada ya kukamilika kwa mchakato wa maoni ya watiania kwenye ngazi za wilaya na mkoa, kimetangaza kuanza mchakato ngazi ya Taifa huku kikisema hadi sasa hakuna aliyekatwa wala kuenguliwa. Dodoma. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuanza rasmi mchakato wa uteuzi wa wagombea ubunge katika ngazi ya Taifa, kikiwataka wote watakaokosa nafasi kuwa watulivu, waaminifu na watiifu kwa chama.
Mpango asisitiza utunzaji kumbukumbu kuzuia upotevu wa dawa
Muktasari: Makamu wa Pili wa Rais, Dk Philip Mpango amesisitiza mambo kadhaa katika kuboresha sekta ya afya Tanzania, ikiwemo kuzitafutia suluhu changamoto za madaktari. Dodoma. Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amesema kutoridhisha kwa hali ya utunzaji wa kumbukumbu dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya na hospitali, kunatatiza usambazaji wa dawa kutoka Bohari ya Dawa (MSD) na kutoa mwanya wa matumizi yasiyo sahihi na wizi.
Sababu za Serikali kupeleka maji Tabora kutoka Ziwa Victoria
Muktasari: Katika kukabiliana na changamoto ya maji mkoani Tabora, Serikali imetaja sababu ya kuachana na kuchimba visima virefu na kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria. Dodoma. Serikali imesema hadi kufikia Julai 2026, changamoto ya maji kwa Mkoa wa Tabora itakuwa historia baada ya mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika wilaya za Urambo, Sikonge na Kaliua kukamilika.
Askofu Kinyaiya atia neno kupumzika Dk Mpango
Muktasari: Januari 18, 2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kukubali ombi la Dk Mpango kupumzika. Dodoma. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma, Beatus Kinyaiya amesema alichofanya Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango kuamua kupumzika si cha kawaida kwa kuwa wengine wanang’ang’ania nafasi za uongozi. Januari 18, 2025 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza kukubali ombi la Dk Mpango kupumzika.
Changamoto zinazoikabili kahawa
Muktasari: Miongoni mwa changamoto hizo ni ucheleweshaji wa malipo kwa wakulima, kushuka kwa ubora wa kahawa, udanganyifu katika mizani, ukosefu wa takwimu sahihi na uuzaji wa kahawa hewa kwenye minada. Dodoma.
Masaju aonya mawakili wanaouza haki za wateja
Muktasari: Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju amewapokea mawakili wapya 449 ikiwa ni tukio la kwanza tangu aapishwe kuishika nafasi hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan, Juni 15, 2025. Dodoma. Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju amewaonya mawakili nchini wenye tabia za kuuza haki za wateja wao kuacha kufanya hivyo, kwa sababu hawatakuwa salama katika maisha yao.
Senene kutegwa na mashine
Muktasari: Serikali imeelezea mafanikio yaliyopatikana Mkoa wa Kagera ikiwemo kufanya utafiti katika uzalishaji wa senene. Dodoma. Wazalishaji wa senene mkoani Kagera wanatarajiwa kuanza kutumia mashine maalumu za wadudu hao mara baada ya kukamilika kwa utafiti, kwa lengo la kuongeza ufanisi katika uzalishaji. Hayo yamesemwa jana Julai Mosi, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwasa wakati akielezea mafanikio ya minne ya Serikali ya awamu ya sita.
Wanafunzi wawili wafariki kwa kufukiwa na kifusi
Muktasari: Kifusi kilichomeguka wakati wakichimba mchanga kilisababisha vifo vya watu wawili. Dodoma. Wanafunzi wawili wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Mbalawala jijini Dodoma wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga wakati wakichimba mchanga Mbalawala jijini Dodoma.
What Tanzanians should expect as new financial year begins
Dodoma. The 2025/26 government financial year officially begins today, July 1, bringing with it a range of changes that offer relief to some citizens while increasing the financial burden on others. The new budget, amounting to Sh56.49 trillion, was passed by Parliament on June 24, 2025. It introduces significant amendments to tax structures, regulatory frameworks, and service charges—some of which will immediately impact the daily lives of Tanzanians.
Kesho kicheko, maumivu
Muktasari: Juni 24, 2025, Bunge lilipitisha bajeti ya Sh56.49 trilioni katika mwaka 2025/26. Bajeti hiyo inayoanza kutekelezwa kesho, inang’ata na kupuuliza kwa wafanyabiashara na bodaboda Dodoma. Mwaka mpya wa Serikali wa 2025/26 unaanza kesho Jumanne, Julai mosi, 2025 kwa bodaboda na wafanyabiashara kufurahia punguzo la tozo, ada huku wanywaji wa vilevi, wachezaji wa michezo ya kubashiri wakianza kuonja joto la kupanda kwa ushuru.
Nderemo na vifijo vyatawala Samia akilifunga Bunge
Dodoma. Ni hotuba iliyosheheni utekelezaji wa sekta mbalimbali. Ndivyo unavyoweza kusema kuhusu hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 ambalo litavunjwa rasmi Agosti 3, 2025. Hotuba ya Rais Samia ya jumla ya saa 2 na dakika 47 ndani ya ukumbi wa Bunge ilikuwa ikikatishwa mara nyingi kwa makofi ya wabunge hata wakati mwingine alilazimika kuwaomba wanyamaze.
Maeneo saba kushindaniwa tuzo za utalii
Muktasari: Tanzania itakuwa mwenyeji wa tuzo za Utalii Duniani kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi kwa mwaka 2025 ambapo maeneo saba kushindaniwa. Dodoma. Serikali imetaja maeneo saba ya ubora yatashindaniwa katika Tuzo za Utalii Duniani Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi kwa mwaka 2025 (World Travel Awards), zitakazofanyika Juni 28, 2025 jijini Dar es Salaam.
ATF yafundwa kupata fedha za afua za Ukimwi
Muktasari: Baada ya Serikali kuanzisha tozo kwa ajili ya kugharamia afya za Ukimwi na Bima ya Afya kwa Wote, imeitaka Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Ukimwi (ATF), kubuni vyanzo vingine vya mapato. Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi ameielekeza Bodi ya Mfuko wa Udhamini wa Ukimwi (ATF) kubuni mbinu za ndani za kutafuta fedha za kugharamia afua za Ukimwi, kufuatia kupungua kwa misaada ya wahisani kwa takriban asilimia 40.
Bunge laridhia kugawa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, uanzishwaji AFC
Muktasari: Bunge limehitimisha mkutano wa 19 wa Bunge la 12, kwa kupitisha maazimio mawili la mkataba wa uanzishwaji wa Shirika la Fedha la Afrika (AFC) na kufanya marekebisho ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Dodoma. Bunge limeridhia azimio la mkataba wa uanzishwaji wa Shirika la Fedha la Afrika (AFC) wa mwaka 2007 ambao unatoa kinga dhidi ya upekuzi, ukamataji, utaifishaji na aina nyingine za kukamata, kuchukua au kuzuiliwa kwa mali za AFC kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi mwanachama.
Mjadala Sheria ya Fedha wahitimishwa kwa ahueni maeneo haya
Prime Muktasari: Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuongeza ushuru wa mazao ambayo Tanzania inajitosheleza. Dodoma. Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2025, Serikali ikifanya marekebisho kwa baadhi ya maeneo yaliyozua mjadala bungeni na miongoni mwa wadau. Miongoni mwa maeneo hayo ni kuhusu ushuru wa bidhaa kwenye huduma za mawasiliano ya kielektroniki na tozo ya dola 44 kwa watalii wanaoingia nchini.
Gambo aibana Serikali kuhusu hatima ya kiwanda cha General Tyre bungeni
Muktasari: Suala la kufufua kiwanda cha matairi ya magari cha General Tyre limekuwa mwiba kwa mawaziri tofauti waliohudumu wakati wa mabunge mawili, huku Serikali ikijinasibu kukifufua. Dodoma. Hoja ya kufufua kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre, imeibuka tena bungeni baada ya Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo, kuhoji mpango wa Serikali kuhusu kiwanda hicho.
Majaliwa ataka taasisi za fedha ziwaamini wachimbaji wadogo
Muktasari: Serikali imezindua mitambo na vifaa vya uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo Tanzania na kuzitaka taasisi za kifedha kupanua wigo kwenye eneo hilo. Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za fedha nchini kuwaamini wachimbaji wadogo kwa kuwapa mikopo ili waondokane na changamoto ya mitaji ambayo walikuwa wanaipata kutokana na kutegemea utabiri wa waganga wa kienyeji katika shughuli zao.
Makalla ataja sababu ya kusitisha ziara na mikutano
Muktasari: Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza sababu ya kusitisha mikutano, ziara, semina na makongamano. Dodoma. Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amosi Makalla, amesema kwamba kusitisha ziara, mikutano na makongamano ni hatua ya kuandaa vizuri mchakato wa uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani ndani ya chama hicho.
Makalla ataja mambo sita watakayofanya uchaguzi mkuu 2025
Muktasari: Mambo mengine ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, kupeleka wagombea wenye sifa, kuheshimiana kwa kutumia utaratibu wa 4R, kutokuwa na kampeni za kubeza wala matusi vyama vingine na kulinda amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Mpwapwa. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ameainisha mambo sita yatakayofanyika katika uchaguzi mkuu ikiwemo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kumtangaza mgombea atakayeshinda kwa haki.
Wiki ya lala salama bungeni, mawaziri…
Muktasari: Juni 27, 2025, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atalifunga Bunge la 12 ambalo lilizinduliwa Novemba 13, 2020 na Rais wa awamu ya tano, hayati Dk John Magufuli. Dodoma. Safari ya miaka takriban mitano ya uhai wa Bunge la 12 unafikia tamati siku tano zijazo, huku ikishuhudiwa mawaziri wakiwa katika kibarua cha kupangua hoja zilizoibuliwa wakati wa mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2025/26.
Vikundi 467 havijaresha mikopo ya asilimia 10 Dodoma
Muktasari: Wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri wakisema sababu ya kusuasua urejeshaji ni watu kupewa mikopo midogo kuliko walichoomba. Dodoma. Vikundi 467 vilivyopewa mikopo ya asilimia 10 ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu havijaresha Sh1.2 bilioni walizopewa na Halmashauri ya jiji la Dodoma.
Wabunge wataka tozo za miamala zipunguzwe
Muktasari: Wasema hatua hiyo itawezesha watu wengi kutumia huduma za miamala ya kieletroniki huku wakibainisha ilipo changamoto. Dodoma. Baadhi ya wabunge wamesema tozo kubwa zinazotozwa kwenye miamala ya kielektroniki kupitia benki na simu zimekuwa kikwazo kwa wananchi, hali inayochangia watu wengi kuepuka kutumia huduma hizo za kifedha.
Mambo 10 ya kuzingatia vijana wanaojiunga JKT
Muktasari: Vijana waliohitimu kidato cha sita na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria mwaka 2025 wameanza leo safari ya miezi mitatu ya kozi hiyo inayotolewa na Jeshi la Kujenga Taifa katika vikosi mbalimbali nchini. Dodoma. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele ametaja mambo 10 ambayo vijana waliojiunga na mafunzo kwa mujibu wa sheria, Operesheni Nishati Safi, wanayopaswa kuzingatia kwa kipindi chote cha mafunzo.
Show More
loading
Actions
Is this you?
As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.Get in touch with Sharon
Contact Sharon, search articles and posts on X, monitor coverage, and track replies from one place.
Learn more about Muck Rack