Is this you? As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.
Claim your profile
Articles by Victor Tullo
Wawekezaji wa China wajipanga kuwekeza Sh200 bilioni Tanzania
Muktasari: Ni kutoka Jimbo la Changzhou, walenga sekta kadhaa zikiwemo za kilimo na afya. Dar es Salaam. Wawekezaji kutoka jimbo la Changzhou nchini China wametenga takribani Sh200 bilioni kwa ajili ya kuwekeza katika sekta mbalimbali hapa nchini, zikiwemo kilimo na afya. Hayo yameelezwa leo Machi 27, 2024 wakati Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lilipokutana na wawekezaji hao kuwaonyesha maeneo wanayoweza kuwekeza.
Ubunifu, teknolojia kubeba dira ya maendeleo 2050
Muktasari: Wadau wa Sekta binafsi nchini wameishauri Tume ya Taifa ya Mipango kukumbatia ubunifu na teknolojia ili kufanikisha utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2050, ambayo mchakato wa kuiandaa umekwishaanza. Dar es Salaam. Wadau wa Sekta binafsi nchini wameishauri Tume ya Taifa ya Mipango kukumbatia ubunifu na teknolojia ili kufanikisha utekelezaji wa dira ya maendeleo ya 2050, ambayo mchakato wa kuiandaa umekwishaanza.
Zungu ataka mazingira yalindwe ili kupunguza joto duniani
Muktasari: Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amesema Kila mtu ana jukumu la kulinda mazingira ili kukabiliana na ongezeko la joto linalosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Dar es Salaam. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, amewataka wananchi wa dini zote kulinda mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Sababu wanafunzi kuchelewa majumbani wakishinda vituo vya daladala, treni
Muktasari: Baadhi ya wanafunzi Dar es Salaam wanachelewa kurudi nyumbani kwa sababu ya ukosefu wa usafiri na kukataliwa na makondakta huku wengine wakidaiwa kuchelewa kwa sababu zao binafsi. Dar es Salaam. Umekuwa ni mtindo wa kawaida kwa baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam kuchelewa kurudi nyumbani wakidai ni ukosekanaji wa usafiri na kukataliwa na makondakta wanapotaka kupanda daladala.
Marekani yang’ata, kupuliza vita vya Israel na Palestina
Muktasari: Misaada ya Marekani huko Gaza imetafsiriwa tofauti huku ikiaminika ni katika harakati za kurejesha imani duniani baada ya kuiunga mkono Israel katika vita vilivyosababisha vifo vya maelfu ya Wapalestina. Dar es Salaam. Tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Palestina huko Gaza Oktoba 7, 2023, Marekani imekuwa mshirika wa karibu wa Israel kwa kutangaza msimamo wa kuiunga mkono. Marekani iliahidi uungaji mkono kwa Israel na msaada wa kijeshi.
VIDEO: Hatua kwa hatua saa 2:20 SGR Dar-Moro
Muktasari: Dar/Moro. Wakati safari rasmi za treni zikitarajiwa kuanza Julai mwaka huu, jaribio la kwanza la treni ya umeme ikiwa na mabehewa manne limefanyika jana kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ikitumia saa 2:20 kufika. Muda huo ni upungufu wa saa 1:40 ya muda wa basi ambao kwa mwendo wa kawaida hutumia saa nne kutoka Dar hadi Morogoro. Treni hiyo ilianza kurudi saa 7:48 na kufika Dar es Salaam saa 10:07, ikitumia saa 2:19.
VIDEO: Hatua kwa hatua saa 2:20 SGR Dar-Moro
Muktasari: Dar/Moro. Wakati safari rasmi za treni zikitarajiwa kuanza Julai mwaka huu, jaribio la kwanza la treni ya umeme ikiwa na mabehewa manne limefanyika jana kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ikitumia saa 2:20 kufika. Muda huo ni upungufu wa saa 1:40 ya muda wa basi ambao kwa mwendo wa kawaida hutumia saa nne kutoka Dar hadi Morogoro. Treni hiyo ilianza kurudi saa 7:48 na kufika Dar es Salaam saa 10:07, ikitumia saa 2:19.
Balozi Kamala afariki dunia
Muktasari: Amefariki dunia jijini Dar es Salaam katika Hospital ya Mzena alipokuwa akipatiwa matibabu. Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa mbunge wa Nkenge na Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala, amefariki dunia leo Februari 12, 2024 katika Hospital ya Mzena jijini hapa alipokuwa akipatiwa matibabu.
Vijana wahimizwa kutumia ujuzi walionao kusaidia jamii
Muktasari: Shirika linalojihusisha na kuhudumia jamii kutokomeza umaskini na kuishi maisha ya staha (My Legacy), limewashauri vijana kutumia ujuzi walionao kuleta mabadiliko. Dar es Salaam. Shirika linalojihusisha na kuhudumia jamii kutokomeza umaskini na kuishi maisha ya staha (My Legacy), limewashauri vijana kutumia ujuzi walionao kuleta mabadiliko.
Makonda anapambana na nani?
Moshi/Dar. Staili ya utendaji kazi wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda kuwananga makada wenzake, watendaji serikalini, wakiwamo mawaziri na vyama vya upinzani, inaibua swali lisilo na majibu kuwa anapambana na nani hasa? Kwa utamaduni uliozoeleka wa siasa za Tanzania, ilitarajiwa katika kukiimarisha chama hicho tawala, Makonda angeelekeza mashambulizi yake kwa vyama vya upinzani pekee, hususani chama kikuu cha upinzani, Chadema, lakini staili yake ni tofauti.
Makonda awataka mawaziri wa viwanda, biashara kutembelea wananchi
Muktasari: Makonda amerudia kusema kuwa akihitimisha ziara yake ya mikoa 20 atawasilisha ripoti wa Rais Samia kuhusu utendaji kazi wa watumishi kwa kila maeneo aliyopita Njombe. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda amemtaka Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji na naibu wake, Exaud Kigahe kufanya ziara katika maeneo mbalimbali nchini ili kusikiliza kero za wafanyabiashara na kuzitolea ufumbuzi.
VIDEO: Sakata la Lissu, Wasafi TV lamwibua Waziri Nape
Muktasari: Waziri Nape Nauye amevitaka vyombo vya habari kutoa uwanja sawa kwa wanasiasa na ameonya dhidi ya kuzuia watu, kitendo alichosema ni kumhujumu Rais Samia. Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nauye amesema hakukuwepo na "maagizo yoyote kutoka juu" katika kuzuia mahojiano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu na kipindi cha Good Morning cha Wasafi TV .
Watumishi saba kampuni ya kukusanya mapato Kinondoni kortini kwa udanganyifu
Muktasari: Wafanyakazi wa kampuni hiyo wameshtakiwa kwa udanganyifu katika ukusanyaji na uwasilishaji wa mapato benki. Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni, imewashitaki wafanyakazi saba wa Kampuni ya Prezidar iliyopewa jukumu la kukusanya mapato na ushuru wa masoko ya Manispaa ya Kinondoni kwa madai ya udanganyifu katika ukusanyaji na uwasilishaji wa mapato benki.
Celine Dion aibukia kwenye tuzo za Grammy
Muktasari: Licha ya kusumbuliwa na ugonjwa adimu wa kukakamaa misuli, mwanamuziki maarufu duniani Celine Dion ameonekana kwenye sherehe za ugawaji wa tuzo za Grammy nchini Marekani usiku wa kuamkia leo jijini Los Angeles, Marekani. Marekani: Mwanamuziki maarufu duniani, Celine Dion ameonekana kwenye sherehe za utoaji tuzo za Grammy 2024 jana Jumapili jijini Los Angeles, Marekani ikiwa ni mara ya kwanza kuonekana hadharani kwa takriban miaka mitatu na nusu.
Moto wa msituni wateketeza watu 112 Chile
Muktasari: Mamlaka nchini Chile imesema takribani watu 112 wamekufa kutokana na moto uliozuka msituni Chile. Takribani watu 112 wamekufa kutokana na moto uliozuka msituni katika eneo la Valparaíso nchini Chile. Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la BBC, Rais wa Chile, Gabriel Boric ametangaza hali ya hatari akisema atatoa mahitaji yote muhimu kukabiliana na madhara yaliyosababishwa na moto huo uliozuka Ijumaa, Februari 2, 2024. Inaelezwa tukio hilo ni baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Kinana: Watanzania changamkieni fursa kituo cha biashara Ubungo
Muktasari: Kituo hicho cha biashara Ubungo kinatarajia kuzinduliwa rasmi kwenye maadhimisho ya Sikukuu ya Sabasaba Julai 7, 2024. Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewataka Watanzania kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye kituo cha biashara cha Ubungo (EACLC) kinachojengwa jijini Dar es Salaam.
Siri shule kongwe za Serikali kupata ufaulu wa juu
Muktasari: Wakati ufaulu ukiongezeka kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka 2023 yaliyotangazwa na Necta jana, baadhi ya shule kongwe za Serikali ni miongoni mwa zilizofanya vizuri, huku takribani asilimia 68 ya wanafunzi wakipata daraja la kwanza. Dar es Salaam. Mwanafunzi mmoja kati ya watatu katika shule 12 kongwe za Serikali amefaulu kwa kupata daraja la kwanza, uchambuzi wa Mwananchi umebaini.
Polisi waimarisha ulinzi maandamano Chadema Dar
Muktasari: Maandamano ya amani ya Chadema yamelenga kuishinikiza Serikali kuondoa miswada ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa bungeni Dar es Salaam. Zaidi ya polisi 20 wameonekana maeneo ya Buguruni yanakoanzia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Karume- Kariakoo - Barabara ya Morogoro kuelekea Barabara ya Sam Nujoma eneo la Ubungo katika Jengo la PSSSF zilipo ofisi za Umoja wa Mataifa (UN).
Polisi waimarisha ulinzi Kariakoo maandamano Chadema
Muktasari: Maandamano ya amani ya Chadema yamelenga kuishinikiza Serikali kuondoa miswada ya sheria za uchaguzi na vyama vya siasa bungeni Dar es Salaam. Ulinzi umeimarishwa na Jeshi la Polisi maeneo ya Kariakoo, huku msafara wa maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) unaoanzia Buguruni ukisubiriwa.
VIDEO: Chadema, Polisi warushia mpira wa maandamano
Muktasari: Hatima ya maandamano hayo itajulikana kesho, polisi watakapotoa taarifa Dar es Salaam. Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisema maandamano yao yanayotarajiwa kufanyika keshokutwa yameruhusiwa na yatalindwa na polisi, jeshi hilo Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema taarifa hiyo si ya kweli. Akizungumza kwa simu leo, Jumatatu Januari 22, 2024, Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema hawajatoa taarifa yoyote ya kuruhusu au kukataza maandamano hayo.
Chadema, Polisi warushia mpira wa maandamano
Muktasari: Hatima ya maandamano hayo itajulikana kesho, polisi watakapotoa taarifa Dar es Salaam. Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisema maandamano yao yanayotarajiwa kufanyika keshokutwa yameruhusiwa na yatalindwa na polisi, jeshi hilo Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema taarifa hiyo si ya kweli. Akizungumza kwa simu leo, Jumatatu Januari 22, 2024, Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro amesema hawajatoa taarifa yoyote ya kuruhusu au kukataza maandamano hayo.
VIDEO: Mama asimulia alivyojiokoa na mwanawe mafuriko Dar
Dar es Saalam. Mvua zilizonyeha jijini hapa kwa siku mbili mfululizo (Jumamosi na Jumapili) zimeacha athari ikiwemo ya watu kukosa makazi huku mama mmoja akisimulia alivyopambana kunusuru uhai wa mwanaye mwenye umri wa wiki mbili. Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumatatu, Januari 22, 2024, mama huyo Jesca Lucas, amesema Januari 20, 2024 (Jumamosi) wakiwa wamelala, walishtushwa na kelele ya watu waliokuwa wakijiokoa na maji yaliyokuwa yameingia na kujaa ndani ya nyumba yao.
Ndege iliyobeba watumishi wa UN yapata ajali, yaua mmoja
Muktasari: Ndege iliyokuwa imekodishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) imepata ajali ilipokuwa ikijaribu kuruka na kugonga jengo na kusababisha kifo cha mtu mmoja. Somalia. Mtu mmoja amefariki dunia huku mwingine akipata majeraha mabaya kufuatia ajali ya ndege ya mizigo katika mji wa Elberde nchini Somalia.
Halmashauri ya Temeke yatishia kufungia stendi binafsi
Muktasari: Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabely amesema wameshatoa notisi kwa wamiliki wa stendi hizo kuhakikisha wanazifanyia usafi na kuziboresha kabla hawajazifunga Dar es Salaam. Wakati Mkoa wa Dar es Salaam ukitangaza maeneo hatarishi yanayoweza kukumbwa na Ugonjwa wa Kipindupindu, Halmashauri ya Wilaya ya Temeke imetishia kuzifungia stendi zinazomilikiwa na watu binafsi watakaoshindwa kuzifanyia ukarabati.
Vita ya Israel, Palestina yaingia siku ya 100, vifo vikizidi 24,000
Muktasari: Zaidi ya watu 24,000 wameuawa tangu kuanza kwa mapigano kati ya Israel na kundi la Kipalestina la Hamas mnamo Oktoba 7 mwaka jana huku vita hiyo ikiingia siku ya 100 leo. . Gaza. Ni siku 100 tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas Oktoba 7, 2023 ambapo adadi ya watu 24,000 wameuawa katika vita hivyo. Zaidi ya watu 23,000 wameuawa Gaza na zaidi ya 59,000 wakijeruhiwa wakati Israel wakiuawa zaidi ya watu 1,000 huku takriban watu 1,000 wakijeruhiwa.
Mataifa zaidi ya 50 kupiga kura mwaka 2024
Muktasari: Mwaka 2024 zaidi ya mataifa 50 yanatarajia kupiga kura katika chaguzi kuu za kitaifa huku hatua hiyo ikitarajiwa kuamua mustakabali wa kisiasa kidunia kwa miongo kadhaa ijayo. Dar es Salaam. 2024 ni mwaka wa uchaguzi duniani, ndivyo unavyoweza kusema, kwani zaidi ya mataifa 50 yakiwamo makubwa ya Marekani na Russia, ayatakuwa na uchaguzi mkuu. Chaguzi hizo zitakazohusisha zaidi ya wapigakura bilioni nne zinatazamiwa kuamua mustakabali wa kasiasa duniani, kwa miaka au miongo kadhaa ijayo.
Wapewa mbinu kuoanisha kazi na majukumu binafsi
Muktasari: Wakati kuoanisha mjukumu ya kazi na maisha mengine ikitajwa kuwa changamoto kwa wafanyakazi wengi, kufanya kazi kutokea nyumbani kumeelezwa kama moja ya mbinu za kumuwezesha mfanyakazi kufanikisha jambo hilo. Dar es Salaam. Kuoanisha kazi na maisha binafsi imekuwa ni changamoto wanayopitia wafanyakazi wengi, hivyo kusababisha kuegemea upande mmoja huku mwingine ukisuasua.
Ajali za mabasi zaua 15, zajeruhi 13 Kenya
Kenya. Watu 15 wamefariki katika ajali iliyotokea leo, Jumanne Januari 9, 2024 asubuhi kwenye barabara kuu ya Nakuru kwenda Eldoret nchini Kenya, ikihusisha basi na daladala. Kwa mujibu wa tovuti ya The Star ya nchini humo, waliofariki katika ajali hiyo ni watu wazima wanane na watoto saba wakiwemo wasichana watano. Kwa mujibu wa Polisi nchini humo, abiria wengine 38 waliokuwa kwenye basi wamenusurika kwenye ajali hiyo huku wenzao 14 waliokuwa kwenye daladala, wamepoteza maisha.
Upinzani DRC wagomea matokeo, muda wa kupinga ukiyoyoma
DRC. Wagombea wa kiti cha urais wa upinzani katika uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamekataa matokeo ya uchaguzi mkuu yaliyotangazwa Jumapili ya Desemba 31, 2023 ambayo Rais Felix Tshisekedi alitangazwa kushinda.
TRC yapokea vichwa vitatu, mabehewa 27 ya SGR
Muktasari: Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Michibia Shiwa amesema TRC inaendelea kupokea kwa awamu vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji wa Reli ya Kisasa (SGR) na wanavijaribu kulingana na matakwa ya mkataba. Dar es Salaam. Shirika la Reli Tanzania (TRC), limepokea vichwa vipya vitatu vya treni za umeme na mabehewa mapya 27 ya abiria na kufanya idadi ya vichwa vilivyopokelewa mpaka sasa kufikia vinne na mabehewa yakiwa 56.
Fedha za HEET zaanza kuleta mabadiliko TIA
Muktasari: Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeshasaini mkataba wa usimamizi na mshauri wa ujenzi wa mabweni mawili katika kampasi ya Mwanza pamoja na kununua vifaa vya Tehama Dar es Salaam. Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), imeanza utekelezaji wa mradi wa mageuzi ya kiuchumi kwa vyuo vikuu nchini (HEET) kupitia Sh27.6 bilioni ilizotengewa, huku ikizindua kamati ya ushauri wa kitasnia katika utekelezaji wa mradi huo.
Waumini watakiwa kusamehe
Muktasari: Waumini katika kanisa la TAG City Christian Center (CCC) Upanga jijini hapa, wametakiwa kuwa na moyo wa kusamehe wakiwemo watoa huduma Tanesco. Dar es Salaam. Waumini katika Kanisa la TAG City Christian Center (CCC) Upanga jijini hapa, wametakiwa kuwasamehe ndugu, rafiki na watoa huduma. Akizungumza katika Mkesha wa kuikaribisha sikukuu ya Krismasi kanisani hapo Mchungaji msaidizi Dk Charles Sokile amesema amani ni jambo la muhimu na ili kuwa nayo waumini hawana budi kusameheana.
Katumbi alia rafu uchaguzi DRC
Muktasari: Mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais nchini DRC, Moise Katumbi ametaka kubatilishwa kwa uchaguzi huo kutokana na kile alichodai kuwa ulitawaliwa na udanganyifu. Dar es Salaam. Mfanyabiashara na mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika Desemba 20, 2023 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Moise Katumbi, ametaka kubatilishwa kwa uchaguzi huo kutokana na kile alichodai kuwa ulitawaliwa na udanganyifu.
70 wauawa kambi ya wakimbizi Gaza
Muktasari: Watu 70 wameuawa katika kambi ya wakimbizi Gaza, idadi hiyo inatajwa huenda ikaongezeka Gaza. Wizara ya afya ya Gaza inayosimamiwa na Hamas imesema shambulizi la anga la Israel limeua takriban watu 70 katika kambi ya wakimbizi ya Al-Maghazi katikati mwa ukanda huo. Taarifa zimesema huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka kutokana na idadi kubwa ya familia zinazoishi katika eneo hilo.
Waumini watakiwa kusamehe, Tanesco yatajwa
Muktasari: Waumini katika kanisa la TAG City Christian Center (CCC) Upanga jijini hapa, wametakiwa kuwa na moyo wa kusamehe wakiwemo watoa huduma Tanesco. Dar es Salaam. Waumini katika Kanisa la TAG City Christian Center (CCC) Upanga jijini hapa, wametakiwa kuwasamehe ndugu, rafiki na watoa huduma likiwemo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Walioibiwa vifaa vya kielektroniki waitwa Polisi kuvitambua
Muktasari: Operesheni maalumu iliyofanywa na Jeshi la Polisi kuanzia Septemba,2023 hadi hivi sasa imesaidia kukamatwa wahalifu 27 na vifaa mbalimbali vilivyoibwa vikiwemo runinga, kompyuta, redio na simu. Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amewataka walioibiwa simu, runinga, kompyuta na redio, kufika kituo Kikuu cha Polisi kuzitambua mali zao zilizokamatwa.
Sababu Serikali kudhibiti kampuni changa
Muktasari: Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amesema lengo la Serikali kuweka udhibiti kwa kampuni change, ni kuzisaidia kukua na kustawi na sio kuweka vizuizi kama ambavyo wengi hudhani. Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew amesema lengo la Serikali kuweka udhibiti kwa kampuni changa, ni kuzisaidia kukua na kustawi na sio kuweka vizuizi kama ambavyo wengi hudhani.
Mabomba mradi wa mafuta EACOP yawasili Dar
Muktasari: Utaratibu wa kuyasafirisha kwenye eneo la mradi waandaliwa, madereva kudhibitiwa kwa mfumo maalumu. Dar es Salaam. Mabomba ya mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda mpaka Chongoleani, mkoani Tanga, Tanzania (EACOP) yameanza kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam.
NEMC yatahadharisha madhara mvua zinazoendelea
Muktasari: Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha nchini, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc) limewatadharisha wananchi, wakiwamo wamiliki wa maeneo ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini kuwa makini ili kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo. Dar es Salaam.
Sh67.7 bilioni kuongeza kampasi ya Chuo Kikuu Ardhi
Muktasari: Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Evaristo Liwa amesema fedha hizo zitatumika kuboresha chuo hicho ikiwamo ujenzi wa kampasi ya Sengerema mkoani Mwanza. Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Evaristo Liwa amesema Sh67.7 bilioni zitatumika katika ujenzi wa kampasi mpya ya chuo hicho wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 378.
Wasichana waongoza ufaulu Ardhi
Muktasari: Wasichana katika chuo kikuu cha Ardhi wameendelea kuibuka vinara kwa ufaulu dhidi wavulana ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo jambo lililotajwa kuleta matumaini katika usawa wa kijinsia katika elimu ya juu. Dar es Salaam. Wasichana katika Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), wameendelea kuibuka vinara kwa ufaulu dhidi wavulana ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo jambo lililotajwa kuleta matumaini katika usawa wa kijinsia katika elimu ya juu.
Moshingi Bosi mpya DCB
Muktasari: Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya DCB, imemtangaza Sabasaba Moshingi kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo kufuatia nafasi hiyo kukaa wazi kwa mwaka mzima. Dar es Salaam. Benki ya Biashara ya DCB, imemtambulisha Sabasaba Moshingi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wake mpya, akijaza nafasi inayoelezwa kuwa wazi kwa “muda mrefu” tangu kuondoka kwa aliyekuwa katika nafasi hiyo.
Rasi: Idadi ya wanafunzi, miundombinu Duce haiendani
Muktasari: Kasi ya ongezeko la wanafunzi katika Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (Duce), haiendani miundombinu iliyopo ya elimu, jambo linatotajwa na mamlaka za chuo kuwa linasababisha mzigo wa kufundisha kuongezeka. Dar es Salaam. Rasi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Profesa Stephen Maluka, ametaja ongezeko la wanafunzi lisiloendana na miundombinu ya elimu iliyopo chuoni hapo, imeongeza mzigo wa kufundisha.
Chalamila ataja manufaa ushirikiano Dar, Shaanxi
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameeleza mafanikio yanayotazamiwa kufuatia makubaliano ya awali yanayohusu mashirikiano kati ya Dar es Salaam na mji wa Shaanxi wa China. RC Chalamila ameeleza hayo Jumatatu, Novemba 27, 2023 Dar es Salaam, kwenye hafla ya utiaji saini makubaliano hayo. Amesema makubaliano hayo ya awali yanalenga ushirikiano kwenye sekta ya viwanda na biashara.
Israel yabadilishana wafungwa kwa mateka
Muktasari: Shirika la Habari la Uingereza (BBC), limeripoti kuwa wafungwa hao waliachiliwa jana Ijumaa Novemba 24, 2023 kama sehemu ya makubaliano yaliyosimamiwa na Qatar, huku yakijumuisha usitishwaji wa mapigano kwa siku nne. Dar es Salaam. Jumla ya wafungwa 39 wa Kipalestina waliokuwa wanashikiliwa katika magereza mbalimbali nchini Israel, wameachiwa huru katika mpango wa kubadilishana wafungwa, mateka baina ya wanamgambo wa Hamas na Israel.
Gharama kubwa, mazoea vyakwamisha matumizi nishati safi
Muktasari: Kwa mujibu wa NBS, zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania wanatumia nishati chafu ya kupikia, sababi zikitajwa kuwa ni gharama kubwa za nishati safi na mazoea mabaya ya watumiaji. Morogoro. Wadau katika sekta ya nishati safi ya kupikia wamebainisha changamoto ya upatikanaji wa nishati hiyo kuwa ni pamoja na gharama kubwa na mazoea mabaya kwa watumiaji kuendelea kutumia nishati chafu ya kupikia.
Waaswa kutumia nishati safi kupikia
Muktasari: Wajasiriamali wanaofanya biashara ya kuuza vyakula maarufu Mama/Baba lishe wameaswa kutumia nishati safi kupikia ili kuokoa muda na kuongeza uzalishaji. Dar es Salaam. Wajasiriamali wanaofanyabiashara ya kuuza vyakula maarufu mama/baba lishe, wameaswa kutumia nishati safi kupikia ili kuokoa muda na kuongeza uzalishaji.
Dk Mollel kula sahani moja na waganga
Muktasari: Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel amewaasa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia maeneo yao kwa uadilifu, huku akisema watawajibika kwa tatizo lolote litakalotokea katika maeneo endapo uzembe ukigundulika. Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amewataka waganga wakuu wa Mikoa na wilaya kuwa waadilifu, akiwaonya kuwa watawajibika kwa uzembe wowote utakaobainika iwapo kutatokea tatizo.
Kisukari chatajwa sababu kuu magonjwa ya figo
Muktasari: Ugonjwa wa kisukari umetajwa kuwa kisababishi kikubw katika kusababisha magonjwa ya figo duniani. Dar es Salaam. Wakati dunia ikiadhimisha wiki ya ugonjwa wa kisukari, ugonjwa huo umetajwa kuwa kisababishi kikuu cha magonjwa ya figo duniani.
Serikali yatafuta fedha kukamilisha ujenzi barabara ya Kimara, Kibaha
KUNRADHI Jumatatu Novemba 13, 2023 katika tovuti hii, tulichapisha habari ambayo ilimnukuu Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akizungumzia kuchelewa kwa ujenzi wa kipande cha Kimara – Kibaha katika Barabara ya Morogoro. Tumefanya uchunguzi na kubaini kwamba maneno aliyonukuliwa Waziri Bashungwa, hakuwa ameyatamka, bali yalisemwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Fanuel Kalugedo.
Show More
loading
Actions
Is this you?
As a journalist, you can create a free Muck Rack account to customize your profile, list your contact preferences, and upload a portfolio of your best work.Get in touch with Victor
Contact Victor, search articles and posts on X, monitor coverage, and track replies from one place.
Learn more about Muck Rack