Habari Jinamizi la kuamua mgombea mwenza wa Ruto 2027 Na JUSTUS OCHIENG July 5th, 2026 Kusoma ni dakika: 3 KINYANG’ANYIRO cha urais wa 2027 kimeanza kushika kasi, lakini nyuma ya pazia kuna pambano jingine lenye uzito mkubwa kumchagua mgombea mwenza. Muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na Rais William Ruto na muungano wa upinzani unaoundwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, Kalonzo Musyoka na washirika wao, wote wanafanya hesabu za kupata mgombea atakayewaongezea nafasi ya ushindi.